Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Mpogolo aipongeza NMB kwa kuanzisha Fanikiwa Account

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo ameipongeza Benki ya NMB kwa kuanzisha akaunti ya Fanikiwa kwani ina lengo la kuwagusa watu wa kipato cha chini ambao ndiyo sehemu kubwa ya wananchi wa Tanzania.
Mpogolo ameyasema hayo baada ya kutembelea banda la benki ya NMB Tanzania kwenye maonesho ya Saba Saba ambapo alipata nafasi ya kupata taarifa kuhusu huduma mbalimbali ambazo zinatolewa na benki hiyo kubwa nchini.
Alisema kuwa akaunti hiyo ni nzuri sababu inawagusa watu wa hali ya chini na maisha ya kati, kundi ambalo linajumuisha sehemu kubwa ya Watanzania na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo kufungua akaunti ya Fanikiwa ili waweze lupata huduma mbalimbali zinapotaikana kwenye akaunti hiyo. 
“Inalenga kuwasaidia watu wa kaiwada kukuza mitaji na kuendeleza kipato chao, mtu anapopata nafasi ya kupata mkopo maana anaweza kuongeza kipato cha familia na ndivyo uchumi wa taifa unavyoweza kujengwa,
“Mimi niwapongeze NMB kwa kuanzisha Fanikiwa Account na niwahamasihe Watanzania watumie fursa hii kuweza kuongeza kipato kwa ajili ya maisha yao na waweze kuongeza kipato,” alisema Mpogolo.
Aidha Mpogolo alizungumza kuhusu baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakihofia kuchukua mikopo kwenye mabenki ili waweze kuongeza kipato, “Ni jukumu la kila mtu kumuhamasiaha mwenzake aone benki ni mahali anapoweza kupata fursa za kujikomboa kiuchumi, kuendeleza ustawi wake mambo kama haya zamani hayakuwepo ambayo yanagusa watu wa hali ya chini,
“Mimi jambo ambalo limenigusa ni kuanzisha akaunti ambayo inagusa watu wa kipato cha chini, naona kwamba Benki ya NMB inakwenda kuwa mkombozi wa watu wanyonge kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais na serikali yake ya kuona wananachi wa kawaida na wao wanaboresha uchumi wao.”
Mkuu wa Kitengo cha Trade Finance ya NMB, Linda Teggisa akimweleza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo kuhusu huduma ambazo zinatolewa na benki ya NMB.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akiuliza jambo kwa Mkuu wa Kitengo cha Trade Finance ya NMB, Linda Teggisa wakati alipotembelea banda la NMB Bank kwenye maonesho ya 41 ya Saba Saba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la NMB Bank kwenye maonesho ya 41 ya Saba Saba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akitoka kwenye banda la NMB Bank kwenye maonesho ya 41 ya Saba Saba.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget