Mkurungezi wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (wa tatu kutoka kushoto)
akipokea kifaa cha sterilizing kutoka kwa Balozi wa Japan nchini
Masaharu Yoshida (kulia). Kutoka Kushosho ni Mkuu wa Idara ya Macho
Muhimbili, Dk Mtemi Baruani na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji
Muhimbili, Dk Julieth Magandi. Kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Kliniki ya
Yamasaki Eye, Dk Takashi Yamasaki na Kenji Takeuchi wa Take Opht Medical
Corporatio. Kifaa hicho kitatumika wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa
wenye matatizo ya macho.
Mkurungezi wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akimshukuru Balozi wa Japan,
Masaharu Yoshida baada ya kuupokea Leo
Mmoja wa wataalamu wa Afya kutoka
Japan, Chika Yoshinda akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa kifaa hicho,
jinsi ya kikutumia na kukitunza.
Baadhi ya wataalamu wa afya kutoka Muhimbili na Serikali ya Japan wakimsikiliza, Chika Yoshinda.
…………………..
Timu
ya Madaktari kutoka nchini Japan kwa kushirikiana na watalaam wa afya
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na MUHAS wanatarajia
kuwafanyia upasuaji wagojwa 30 wenye matatizo ya mtoto wa jicho.
Akipokea
msaada wa kifaa cha utakasaji ( Sterilizing instruments ) pamoja na
vifaa mbalimbali vitakavyotumika wakati wa upasuaji huo (Consumables )
kutoka kwa timu ya wataalam wa afya wa nchini Japan , Mkuruenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru
amesema zoezi hilo la upasuaji litafanyika kesho na keshokutwa .
‘’Tumekua
na ushirikiano mzuri na wataalam hawa kwa muda wa miaka 12 sasa na
niamini ushirikiano huu utaendelea, lakini pia uwepo wa Madaktari hawa
utusaidia kuwajengea uwezo watalaam wetu hapa Muhimbili,” . Amesema
Profesa Museru.
Profesa
Museru amesema msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo MNH ina
mahitaji ya vifaa mbalimbali vya vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia
wagonjwa .
Kwa
upande wake Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida amesema nchi yake
itaendelea kushirikiana na MNH katika kuboresha huduma za afya na
kudumisha ushirikinao huo wa kihistoria.
Post a Comment