Wanawake
wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama cha
Mpira wa Miguu Wanawake (TWFA) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika
Julai 8, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi
ya TWFA, Msomi Wakili George Mushumba leo Juni 23, aliongoza kikao cha
Kamati ya Uchaguzi kupitia majina ya wagombea walioomba kugombea nafasi
mbalimbali.
Mara baada ya kikao hicho,
amewataja wanaowania nafasi mbalimbali kwenye mabano kuwa ni Amina
Karuma (Nafasi ya Uenyekiti); Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti); Somoe
Ng’itu (Katibu) na Theresia Mung’ong’o (Katibu Msaidizi ).
Nafasi ya Mweka Hazina, kwa
mujibu wa Mushumba inawaniwa na Hilda Masanche ilihali nafasi ya Ujumbe
wa Mkutano Mkuu TFF, inawaniwa na Salma Wajesso na Zena Chande huku
Ujumbe wa Kamati ya Utendaji TWFA waliopitishwa ni Triphonia Temba,
Jasmine Badar, Chichi Mwidege na Mwamvita Kiyogomo.
Musumba ametangaza majina hayo ya
wagombea waliostahili au waliotimiza taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa
katiba na kanuni za uchaguzi za TWFA.
Kinachofuata kwa sasa ni kwamba
Juni 26 na 27, 2017- Kupokea pingamizi kati ya saa 4:00 asubuhi hadi saa
10:00 jioni katika ofisi za TFF.
Juni 28, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia pingamizi kama zimewasilishwa.
Juni 29, 2017- Kamati kutoa majumuisho ya pingamizi kama ziliwasilishwa na wadau.
Juni 30, 2017- Usaili kwa wagombea waliotangazwa.
Julai 01, 2017- Kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa
Julai 02, 2017-Kamati kupokea rufaa
Julai 03, 2017- Kamati kupitia rufaa kama zimewasilishwa.
Julai 04, 2017 Kamati kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea.
Julai 04 hadi 07, 2017 – Wagombea kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili.
Julai 08, 2017- Uchaguzi Mkuu wa TWFA
Post a Comment