Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira
wa Tanzania (TFF), imetangaza Uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo
utakafanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma.
“Napenda kuwatangazia wadau wote wa mpira
wa miguu kuwa mnakaribishwa kugombea nafasi zilizo orodheshwa hapo chini
kwa kuchukua fomu Ofisi za TFF Karume Ilala na pia unaweza kuzipata
katika tovuti ya TFF: www.tff.or.tz,” amesema Kuuli.
Akitangaza tarehe hiyo mbele ya
wanahabari, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus
Kuuli, amesema kwamba kamati yake haitakuwa na huruma kwa ishara yoyote
ya rushwa katika kipindi chote cha uchaguzi.
Wakili Kuuli amesema kamati yake itandesha
uchaguzi huo kwa Uhuru na Haki na kuzingatia taratibu, kanuni na sheria
zote zilizopo.
Kuuli, amesema Kamati yake itafanya kazi
na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) na jeshi la Polisi kuhakikisha uchaguzi huo
hautakuwa na vitendo vya rushwa.
“Tunawatahadharisha wagombea woye kukaa
mbali na vitendo vya rushwa…, kamati yetu haitakubali vitendo hivyo na
tutafanya kazi na mamlaka za Serikali kuhakikisha yeyote atakayehusika
na vitendo hivi anachukuliwa hatua, Takukuru wataufuatilia kwa karibu
uchaguzi huu,” alisema Kuuli.
Akizungumzia mchakato mzima, Kuuli
anasema, mchakato wa kuchukua fomu na kuzirejesha ni Juni 16 mpaka 20,
mwaka huu na kikao cha mchujo wa awali kwa wagombea kitafanyika Juni 21
mkapa Juni 23.
Juni 24 na 25, mwaka huu, kamati itafanya
kazi ya kuchapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo majina ya
wagombea wakati Juni 26-28 zitakuwa siku za kupokea na kuweka
mapingamizi kwa wagombea na Juni 29 mpaka Julai Mosi itakuwa kipindi cha
kupitia mapingamizi yote na kufanya usaili.
Kwa mujibu wa Kuuli, Julai 2-3 kitakuwa
kipindi cha kuchapisha na kubandika matokeo ya usaili, Julai 4-7 na
kipindi cha Sektretarieti kuwasilisha masuala ya Kimaadili kwenye Kamati
ya maadili, Julai 7-11 ni kipindi cha kusikiliza na kutolea maamuzi
masuala ya kimaadili.
Julai 15-17 kitakuwa kipindi cha kukataa
Rufaa kwa maamuzi ya masuala ya kimaadili kwenye kamati ya rufaa ya
Maadili ya TFF, Julai 18-22 itakuwa siku ya kusikiliza rufaa za maadili
na Julai 23 mpaka Julai 25 itakuwa siku ya kutoa maamuzi ya Rufaa, Julai
26-28 kitakuwa kipindi cha kukata rufaa dhidi ya kamati ya Uchaguzi
kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF, rufaa hizo zitasikilizwa
Julai 29 mpaka Agosti 2.
Wagombea watajulishwa matokeo ya Kamati ya
Uchaguzi ya TFF na Agosti 5-6 itakuwa siku ya kuchapisha majina ya
wagombea watakaoingia kwenye Uchaguzi huo na kampeni kwa wagombea
zitaanza Agosti 7 mpaka 11 na siku inayofuata yaani Agosti 12 itakuwa
siku ya uchaguzi wa viongozi wa TFF.
Nafasi zinazogombewa ni Rais wa TFF,
Makamu wa Rais pamoja na nafasi 13 za wajumbe TFF wanaowakilisha kanda
13 za Kagera na Geita;
Mara na Mwanza;
Shinyanga na Simiyu;
Arusha na Manyara;
Kigoma na Tabora;
Katavi na Rukwa;
Mbeya na Iringa;
Njombe na Ruvuma;
Lindi na Mtwara;
Dodoma na Singida;
Pwani na Morogoro;
Kilimanjaro na Tanga na
Dar es Salaam ambayo ni kanda pekee.
Sifa za wagombea
GHARAMA ZA KUCHULIA FOMU.
1. Rais TSHS 500,000/=
2. Makamu wa Rais TSHS 300,000/=
3. Wajumbe wa kamaki ya utendaji TSHS 200,000/-
SIFA ZA WAGOMBEA.
- 1. Awe raia wa Tanzania.
- 2. Awe na kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne (Cheti cha Elimu ya Sekondari).
- 3. Awe na uzoefu wa uendeshaji Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano.
- 4. Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na asiwe amewahi kuhukumiwa kifungo kisicho na mbadala wa faini.
- 5. Awe na umri angalau miaka 25.
- 6. Awe amewahi kuwa ama Mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi. Au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu angalau katika ngazi ya Mkoa au ngazi ya daraja la kwanza.
- 7. Awe muadilifu na muaminifu mwenye uwezo wa utendaji katika utekelezaji na utimizaji wa majukumu na malengo ya TFF.
- 8. anayegombea nafasi ya Rais au makamu wa Rais awe na kiwango cha elimu kisichopungua shahada moja, mwenye utu na uwezo wa kuiwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 16-20/06/2017 saa kumi (10:00) jioni.
MCHAKATO MZIMA WA UCHAGUZI NI KAMA UFUATAVYO:
1 | 14-15/06/2017 | Kutangaza mchakato wa Uchaguzi wa TFF nafasi zinazogombewa na kubandika kwenye mbao za matangazo | Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi TFF | 10.7 | 2 |
2 | 16-20/06/2017 | Kuanza kuchukua fomu za kugombea. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu za kuomba uongozi. | Wagombea wote | 10.8 | 5 |
3 | 21-23/06/2017 | Kikao cha mchujo wa awali wa wagombea na Kuandika barua za Kuwajulisha wagombea juu ya mchujo wa awali | Kamati ya Uchaguzi TFF | 11.1 | 3 |
4 | 24-25/06/2017 | Kuchapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea | Kamati ya Uchaguzi TFF | 11.2 | 2 |
5 | 26-28/06/2017 | Kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea | Wagombea | 11.3 – 4 | 3 |
6 | 29/6-1/7/2017 | Kupitia pingamizi zote na kufanya usaili wa wagombea | Kamati ya uchaguzi na Wagombea | 11.7 | 3 |
7 | 02-03/07/2017 | Kutangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo Matokeo ya awali ya usaili | Kamati ya Uchaguzi TFF | 11.8 | 2 |
8 | 04-06/07/2017 | Sekretariati kuwasilisha masuala ya kimaadili kwenye kamati ya Maadili | Kamati ya maadili ya TFF | 11.10 | 3 |
9 | 07-11/07/2017 | Kipindi cha Kupokea na kusikiliza na kutolea Maamuzi masuala ya maadili | Kamati ya Maadili ya TFF | 11.10 | 5 |
10 | 12-14/07/2017 | Kutangaza matokeo ya maamuzi ya kamati ya Maadili | Kamati ya Maadili ya TFF | 11.10 | 3 |
11 | 15-17/07/2017 | Kipindi cha kukata Rufaa kwa Maamuzi ya Masuala ya Kimaadili kwenye kamati ya rufaa ya Maadili ya TFF | Wagombea | 11.11 | 3 |
12 | 18-22/07/2017 | Kusikiliza rufaa za kimaadili | Kamati ya rufaa ya maadili ya TFF na Wagombea. | 11.12 | 5 |
13 | 23-25/07/2017 | Kutoa maamuzi ya Rufaa | Kamati ya rufaa ya maadili ya TFF. | 11.12 | 3 |
14 | 26-28/07/2017 | Kipindi cha Kukata Rufaa Dhidi ya Kamati ya Uchaguzi kwenye kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF | Wagombea na Katibu Mkuu TFF. | 13.1 | 3 |
15 | 29/7-2/8/2017 | Rufaa kusikilizwa na kamati ya rufaa ya Uchaguzi ya TFF | Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF na Wagombea | 13.2 | 5 |
16 | 03-04/08/2017 | Wagombea na kamati ya uchaguzi kujulishwa maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF | Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF | 13.3-4 | 2 |
17 | 05-06/08/2017 | Kuchapisha orodha ya Mwisho ya Wagombea na kutangazwa na kubandikwa kwenye mbao za matangazo | Kamati ya uchaguzi TFF. | 14.1 | 2 |
18 | 07-11/08/2017 | Kipindi cha kampeni kwa wagombea | Wagombea | 14.3 | 5 |
19 | 12/08/2017 | Uchaguzi Mkuu wa TFF | Wagombea Wajumbe na Kamati ya Uchaguzi TFF |
14.4
|
1 |
Post a Comment