Wakuu wa Idara wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakijadili masuala mbalimbali
walipotembelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Bw. Ramadhan
Maleta, katika mwanzo wa Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23
kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhani Maleta akimsikiliza
na Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA), Bw.Joseph Nyahende (kushoto), wakati wa kuadhimisha
Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16 hadi 23. Wa pili kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu, Bw. Mohamed Ally na kushoto ni
Mkurugenzi Viwanja vya Mikoa, Bw. Valentine Kadeha.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama
katika jengo la kuwasili na kuondokea abiria mashuhuri la VIP kwenye
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Leonard
Mbogoma (wapili kushoto)akimuelezea jambo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhan Maleta
alipotembelea jengo hilo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma iliyoanza Juni 16-23.
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Joseph Nyahende
akimfafanulia jambo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhan Maleta ikiwa ni siku ya kwanza ya
Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23.
Ofisa Biashara wa JNIA, Bi.
Herrieth Nyarusi (kushoto) akizungumza wakati Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhan Maleta
alipotembelea Idara ya Biashara kusikiliza kero na maoni kutoka kwa
watumishi, ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Kulia ni
Meneja wa Fedha (JNIA), Bw.Shadrack Chilongani na katikati ni Bw.
Godfrey Kanyama.
Post a Comment