Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la
mbeya wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya
Utumishi na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi (hayupo pichani) alipofanya
ziara jijini hapo mapema leo lengo ikiwa ni kusikiliza changamoto
wanazokutana nazo waajiri katika Utumishi wa Umma na kuzipatia ufumbuzi.
Ziara hiyo ni moja ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya
Bw. Musa Mapunda (wa pili kutoka kushoto) akieleza majukumu ya jiji hilo
wakati wa kikao kati ya viongozi wa Jiji hilo na Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan
Mlawi (kulia) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
2017.
Kaimu Katibu Tawala wa Jiji la
Mbeya Bw.Nyasembwa Sivangu akisoma taarifa ya Jiji la Mbeya wakati wa
kikao kati ya viongozi wa Jiji hilo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi (wa
pili kutoka kulia) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma 2017. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri kazi Ofisi
ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi akitoa
ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa viongozi wa Halmashauri ya Jiji
la Mbeya alipofanya ziara ofisini hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
wiki ya utumishi wa umma 2017.
Mmoja wa watumishi wa
Halmashauri ya Jiji la Mbeya akiuliza swali wakati wa ziara ya Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi
(hayupo pichani) jijini hapo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma 2017.
Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la
Mbeya wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi (hayupo pichani) wakati
wa kikao kilichofanyika mapema leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
wiki ya utumishi wa umma 2017
Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na
Ushauri kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba,akitoa ufafanuzi
kuhusu ujazaji wa fomu za OPRAS zinazopima utendaji kazi wa mtumishi.
Post a Comment