Kamishna wa Ardhi msaidizi –
Kanda ya Kati (Dodoma); Hezekiel Kitillya akizungumza na Waandishi wa
habari kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi yake, Tathimini ya Malipo
ya Kodi ya Pango la Ardhi ya Kanda na Maboresho ya ulipaji wa Kodi hiyo
kwa njia ya Kielektroniki. Kushoto kwake ni Mwanasheria na Afisa Ardhi
mwandamizi; Jane Kapongo na kulia kwake ni Msajili wa Hati katika kanda
hiyo; Geoffrey Mauya.
Vipeperushi vya kuelimisha jamii kuhusu Kodi ya Pango la Ardhi vikigaiwa kwa Wananchi katika Stand ya Mabasi mjini Dodoma
Kamishna wa Ardhi msaidizi –
Kanda ya Kati (Dodoma); Hezekiel Kitillya akizungumza na A Fm Radio –
92.9 – Dodoma; kuhusu Tathimini ya Malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi ya
Kanda na Maboresho ya ulipaji wa Kodi hiyo kwa njia ya Kielektroniki.
Kamishna wa Ardhi msaidizi –
Kanda ya Kati (Dodoma); Hezekiel Kitillya akizungumza na Maisha Radio –
100.1 – Dodoma; kuhusu Tathimini ya Malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi
ya Kanda na Maboresho ya ulipaji wa Kodi hiyo kwa njia ya Kielektroniki.
………………………………………………
Kanda ya kati (Dodoma) yakusanya
kiasi cha Tshs. 1,426,273,033.70 ya Makusanyo ya Kodi ya Pango la Ardhi,
sawa na 204% ya malengo na hivyo kuvuka malengo iliyopangiwa. Kamishna
Msaidizi wa Ardhi, kanda ya kati Dodoma; Hezekiel Kitillya ameeleza
wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.
Kamishna Kitillya alisema;
tathimini iliyofanyika ni ya mpaka 31 Mei, 2017. Malengo ya Makusanyo
yaliyokuwa yamepangwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 – 30 Juni, 2017 yalikuwa ni
kukusanya kodi ya Tshs. Bilioni 111.77, ambapo kati ya kanda nane za
ardhi zilizopo nchini, kanda ya kati ilipangiwa kukusanyaTshs. Milioni
700.
Vile vile, baadhi ya Halmashauri
tayari zimeshavuka malengo ya makusanyo zilizowekewa, kama vile
Manispaa ya Dodoma, malengo yalikuwa Tshs. 200,000,000/= na makusanyo
yakawa; Tshs.678,804,841.40, Manispaa ya Singida, malengo yalikuwa
Tshs. 200,000,000/= na makusanyo yakawa Tshs.308,392,069.17 na
Halmashauri ya Manyoni, malengo yalikuwaTshs. 100,000,000/= na makusanyo
yakawa Tshs. 117,200,000.00. Pia Halmashauri nyingine za Wilaya ya
Itigi, Chamwino, Bahi; nazo zimeshavuka malengo na nyingine zilizobaki
zikikaribia kufikia malengo.
Akieleza moja ya mkakati muhimu ambao umewezesha kanda yake kuvuka malengo ni pamoja na kusambaza hati za madai Demand notes. Alisema; “Halmashauri zote zilielekezwa kuandaa na kusambaza hati za madai kwa wadaiwa wakubwa sugu”.
Akizungumzia moja ya changamoto
Kuu inayokabili zoezi la Makusanyo; Alisema ni Wananchi kutokuwa na
uelewa wa kutosha kuhusu tofauti ya Kodi ya Pango la Ardhi na Kodi ya
Majengo, ambapo Wananchi wengi hudhani wakishajenga nyumba na kuanza
kulipa kodi ya jengo, hawapaswi tena kulipa kodi ya pango la Ardhi.
Aidha, Kamishna Kitillya ametoa
wito kwa Wananchi kuhamasika kulipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa mujibu wa
Sheria na kwa Maendeleo ya Taifa. Aliongeza kuwa; “Sasa Kodi ya Pango
la Ardhi imeboreshwa kwa kumuwezesha mwananchi kutambua kiasi
anachodaiwa na kufanya malipo hayo kieletroniki, kwa kutumia Tovuti ya
Wizara au simu kwa tigo pesa au m-pesa, tofauti na ilivyokuwa awali
ambapo Mwananchi alilazimika kufika katika vituo vya malipo, katika
Halmashauri yake”.
Kanda yakati (Dodoma) inahudumia mikoa miwili (2) Dodoma na Singida yenye jumla ya Halmashauri kuminatano (15).
Post a Comment