Mwagala
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni ,Benjamini Sitta akizungumza wakatiwa
kikao cha baraza la Madiwani katika ukumbi wa Manispa ahiyo Magomeni
jijini Dar es Salaam, juni 15, 2017.
Na Humphrey Shao
Baraza
la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni limeagiza kuhakikisha fedha zote
zilizopo katika akaunti za kata zaidi ya Bilioni 4.9 zifanyiwe utaratibu
wa manunuzi ili ziweze kutekeleza miradi iliyokusudiwa katika kata
hizo.
Maazimio hayo yamefikiwa katika
baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo lililongozwa na Mstahiki Meya wa
Manispaa hiyo, Benjamini Sitta .
Aidha
baraza hilo pia limeridhia maombi ya kamati ya Fedha kwa kutaka kubuni
vyanzo vipya vya fedha vitakavyosaidia Halmashauri hiyo kupata fedha
zaidi licha ya baadhi ya vyanzo kuhamia serikali kuu.
pia
kikao hicho kilipitisha azimio la kumpongeza Rais John Pombe Magufuli
kwa kitendo chake cha kizalendo cha kuhakikisha kuwa fedha za watanzania
zilikuwa zinapotea kutokana na mchanga wa Madini uliokuwa ukisafirishwa
nje kiholela unapangiwa utaratibu wa kunufaisha Serikali.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ,Aron Kangurumjuli aakizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo akichangaia katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Kinondoni.
Post a Comment