MEYA MSTAAFU YUSUFU MWENDA AWATAKA VIONGOZI WENYE UWEZO KUWASAIDIA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda amewataka wananchi, taasisi na viongozi mbalimbali wenye uwezo kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa lengo la kuwakwamua na hali ya kiuchumi iliyopo kwa sasa.
Mwenda ameyasema hayo Jijini Dar es salaam jana katika hafla ya Idd aliyoindaa nyumbani kwake na kusheherekea na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni.
Alisema pamoja na mambo mengine,kufanya hivyo ni kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika harakati zake za kimaendeleo anazozifanya.
Alisema viongozi wananchi pamoja na jamii kwa ujumla haina budi kuendana na dhamira aliyonayo Rais Magufuli ya Taifa kujikwamua kiuchumi hususani kipindi hiki anapofanya mambo mbalimbali ya kuliletea maendeleo.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akizungumza wakati wa hafla ya Idd aliyoindaa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. na kusheherekea na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni .
Mratibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Imra James Gabon akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea msaada.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akiwakabidhi watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni .baadhi ya zawadi aliyowaandalia (kushoto) Mratibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Imra James Gabon.
Mke wa Meya Mama Tausi Yusufu Mwenda (mwenye nguo ya bluu) akimkabidhi moja ya zawadi Bi.Nuhimu Iddi anayetoka katika kituo hicho.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akiwakabidhi zawadi watoto
Post a Comment