MWAGALA
Guest of
honor Lord Mayor of Dar es salaam city Isaya Mwita delivering a
speech during a commemorating the UN road safety week today at Upanga
Dar es salaam Director and CEO of AAT Mr Yusuf Ghor speeking to Invited Guest during the function of the program of installing appropriate road signs near the schools to save the lives of students .
NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amewataka madereva
wanaowasafirisha wanafunzi wanaosoma shule nilizopo katikati ya jiji
kuwashusha na kuwachukua ndani ya kuta za shule badala ya kuwashusha
na kuwachukua nje.
Meya
Mwita aliyasema hayo jijini hapa leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya
Kimataifa ya usalama barabarani ,ambapo pamoja na mambo mengine alisema
kuwa utaratibu wanaoutumia madereva hao ni hatari kwa wanafunzi kwani
inawalazimu kuvuka barabara.
Alisisitiza
kuwa iwapo watatumia utaratibu wa kushusha wanafunzi ndani ya kuta za
shule itasaidia kupunguza hatari kwa wanafunzi ikiwemo kugongwa na gari,
pikipiki, kupunguza msongamano wa magari barabarani.
"
Jambo ambalo linakwenda kufanyika leo ni muhimu sana, limesaidia
kuongeza usalama wa watoto wetu ambao wanasoma kwenye shule hizi
zilizopo katikati ya jiji, lakini pia linatoa nafasi kwa walimu kuwa na
uhakika wa usalama wa wanafunzi wao, najua wakati mwingine mmekuwa na
wasiwasi kuhusu usalama wao.
"
Nipende kutoa rai kwa madereva, zingatieni jambo hili , mabasi ya shule
yawe yanachukua na kushusha wanafunzi ndani ya kuta za shule ,
utaratibu ambao mlikuwa mnautumia hivi sasa usitishwe mara moja.
Huko
ni kuhatarisha maisha ya wanafunzi , ambao badae wangekuwa madokta ,
wabunge, marais , ndio ambao tunawategemea , watoto ndio Taifa la kesho,
nawaomba sawa , walimu mlisimamie jambo hilo,
Aidha
Meya Mwita aliwataka walimu na shule kwa ujumla kutumia kwa umakini
vifaa vya usalama barabarani katika mitaala ya shule ili kuwafundishia
wanafunzi masuala ya usalama barabarani kwani kutafanya watambue elimu
hiyo na hivyo kuleta manufaa kwa Taifa.
Alisisitiza
kuwa " elimu hii ikifundishwa vizuri itapunguza ajali za barabarani
wakati wa kuvuka lakini pia hata pikipiki zitaendeshwa kwa kuzingatia
sheria za usalama barabarani ,bila kuathiri watumiaji wengine wa
barabara.
Hata hivyo Meya
Mwita aliwapongeza Automobile Association Of Tanzania (AAT), na
Federation International Automobile (FIA) kwa kuchukua jukumu la
kupunguza ajali barabarani na kuokoa maisha ya wanafunzi.
AIdha
AAT, FIA kwa kushirikiana na kitengo cha Usalama barabarani elimu kwa
umma, wamefundisha walimu 1000 kutoka shule 51 za jiji la Dar es Salaam
kuhusu matumizi sahihi ya alama za barabarani na matumizi sahihi ya
barabara ambapo matarajio yake ni kuwafikia wanafunzi wengizaidi.
Sambamba
na hilo , AAT, FIA imeahidi kutoa elimu hiyo kwa kila halmashuri za
jiji la Dar es Salaam ambapo jumla ya watu 10 watakuwa wakipatiwa
mafunzo hayo.
Post a Comment