Mkuu
wa mkoa wa Iringa bi Amina Masenza akiwa sambamba na katibu tawala wa
mkoa wa Iringa bi wamoja Ayoub wakiwa katika viwanja vya Ikulu ndogo
wakifurahia jambo baada ya futari ya pamoja wa watu zaidi ya miambili
Baadhi ya watu waliojitokeza kushiriki futari pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza.
Na Fredy Mgunda, Iringa
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Amina masenza amefutulisha futari watu zaidi ya mia
mbili katika eneo la Ikulu iliyopo kata ya gangilongo kwa lengo
kudumisha amani na upendo.
Akizungumza
baada ya futari Mkuu wa mkoa masenza aliwataka waumini wote wa dini ya
kiislamu na wakristo kuwa makini katika maeneo ya ibada ili kuepukana na
kutoka kwa shambilio lolote lile ambalo litasababisha maafa.
“Tumeona
nchi nyingine kipindi hiki cha ramadhan kukitokea milipiko mingi ya
kujitoa mhanga kwa baadhi ya watu wenye itikadi kali hivyo tunapaswa
kuwa makini mno mwezi huu hata miezi mengine yote kwa kudumisha amani
yetu”alisema Masenza
Masenza
aliwaomba wananchi wote wa mkoa wa Iringa kuwafichua waalifu wanaofanya
shughuli hiyo kwa njia yoyote ile ili kuendelea kudumisha tunu
tuliyokuwa nayo toka wakati tunapata Uhuru hadi hii Leo.
Aidha
Masenza aliwaomba watanzania kuendelea kumuunga mkono na kuombea Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe Magufuli katika vita
hii ya kukuza uchumi kutoka hapa tulipo hadi uchumi wa kati kwa kuwa
vita hii sio lelemama.
“Ni
kitu kigumu sana unapogusa maslai ya mtu binafsi kwa maslai ya wanyonge
huwa inakuwa vita kubwa kupambana nayo lakini Rais wetu mpendwa
anafanikiwa hilo hivyo lazima tuwe tunamuombe na kumuunga mkono ili
tuendelee kumpa moyo kwenye vita hii” alisema Masenza
Niwaombe
wananchi wa mkoa wa Iringa kuwapuuza viongozi wanaopotosha ukweli wa
mambo ambayo serikali inayafanya kwa manufaa ya wananchi wa kipato cha
chini,kati na wale wenye kipato kikubwa pasipo kumnyang’a au kumdhulumu
mtu haki yake.
Katika
futari hiyo kulihudhuriwa na wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Iringa
kama Kilolo iliwakilishwa na mh Asia Abdalah,Mufindi Jamhuri William na
wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Lakini
mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah aliwataka wananchi na viongozi
kutunza amani na kuacha kufanya uharifu kipindi hiki cha ramdhan hata
baada ya kuisha ramadhan ili kuendelea kuweka nchi kwenye utulivu uliopo
sasa.
“Unakutana
na mtu kipindi hiki anajifanya kafunga lakini matendo yake hayaendani
ya wakati uliopo lakini kuna wengine saizi wametulia ila ramadhan
ikiisha tu anaanza matendo ya uvunjifu wa amani hivyo niwaombe tena na
tena wananchi kutunza amani iliyopo “alisema Abdalah
Abdalah
alimshukuru mkuu wa mkoa wa Iringa bi Amina masenza kwa futari ambayo
imewakutanisha watu mbalimbali kukaa pamoja na kubadilisha mawazo japo
kwa muda mchache hivyo kuwaomba wakuu wenzake wa wilaya zote za mkoa wa
Iringa kuiga mfano wa mkuu wa mkoa.
Nao
baadhi ya viongozi wa dini waliofika eneo la futari walimpongeza mkuu
wa mkoa kwa kufutulisha watu mbalimbali ambao imekuwa fursa ya kufanya
wabadilishane mawazo ya kujenga tofauti na kila mmoja angefuturu kwake.
“Hili
ni jambo jema sana kwa kiongozi wetu wa mkoa maana leo tumekutana na
viongozi kutoka dini mbalimbali hata wengine sio viongozi lakini
tumebadishana mawazo na hili ni jambo jema kwetu sisi kwa ukweli
tumejifunza mambo mengi leo mungu ambariki mheshimiwa mkuu wa mkoa”
walisema viongozi wa dini
Post a Comment