Waziri wa Kilimo,Maliasili Mifugo
na Uvuvi Hamad Rashid kushoto akibadilishana mawazo na Waziri wa Fedha
na Mipango Dk,Khalid salum Mohammed katika baraza la Wawakilishi
Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni
na Michezo Rashid Ali Juma akibadilishana mawazo na Muakilishi wa Jimbo
la Kikwajuni Nassor Salim Ali katika baraza la Wawakilishi Zanzibar.
-Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya Ufungaji wa Baraza la
Wawakilishi ilioambatana na uchambuzi wa masuala mbalimbali
yaliojadiliwa katika baraza hilo Mbweni Zanzibar.
-Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya Ufungaji wa Baraza la
Wawakilishi ilioambatana na uchambuzi wa masuala mbalimbali
yaliojadiliwa katika baraza hilo Mbweni Zanzibar.
……………………………………………………………
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imewataka Wananchi ambao wanadai kuchukuliwa maeneo yao kufuatia zoezi
la kuzuia Mchanga wawasilishe Vielelezo vyao katika Taasisi husika ili
kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.Hayo yamesemwa
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika hotuba
yake ya kuahirisha kikao cha Tisa cha Baraza la Wawakilishi mbweni nje
kidogo ya mji wa Zanzibar.
Amesema hatua iliyochukuliwa
ilikuwa na lengo la kuweka utaratibu mzuri wa matumizi bora ya Mchanga
ambao kadri unavyotumika unaendelea kumalizika.Balozi amesema Serikali
imeandaa utaratibu ambao kama utafuatwa vyema utaweza kuinusuru Zanzibar
na uhaba wa mchanga kwa vizazi vya sasa na baadae.
Kuhusu malalamiko yanayotolewa na
Wananchi juu ya utendaji wa Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja Balozi amesema
kuanzia sasa Serikali haitomvumilia mfanyakazi yeyote atakayefanya
uzembe na hatua kali za kinidhamu ama kufukuzwa kazi zitachukuliwa dhidi
yake.
Amesema yapo malalamiko kuwa
baadhi ya madaktari hushindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo na
kuwatolea lugha chafu wagonjwa jambo ambalo si haki na halivumiliki
tena.Amesema dhamira ya Serikali ya Mapinduzi chini ya Dkt Ali Mohamed
Shein ni kutoa huduma bora za afya nchini na kuahidi kuyafanyia kazi
mapungufu yaliyobainishwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa uzito
wake.
Kuhusu Michezo Balozi Seif
amesema Serikali inaendelea na juhudi zake za kuimarisha michezo nchini
na kuwapongeza waliosaidia harakati za Zanzibar kupata uanachama wa
kudumu wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).
Amesema kufuatia Zanzibar kupata
uanachama huo wa CAF kunaashiria uwezekano mkubwa pia wa kupata
Uanachama wa FIFA hali ambayo itapelekea Vijana kushiriki katika
mashindano ya kimatifa.Ameongeza kuwa tayari hatua za awali za kuomba
uanachama wa FIFA zimeshaanza kuchukuliwa na Serikali na kwamba kazi
iliyonayo ni kuwaandaa Vijana kushiriki mashindano hayo.Katika Mkutano
huo wa tisa Baraza lilijadili na kupitisha Bajeti ya serikali ambapo pia
jumla ya maswali 169 ya msingi na Maswali 418 yanyongeza yaliulizwa na
kupatiwa majibu. Aidha mkutano huo ulijadili jumla ya Miswada mitano na
kuipitisha kuwa sheriaKwa upande wake Spika wa Baraza la Wawakilishi
Zubeir Ali Maulid aliwataka wajumbe wa Baraza hilo kurudi Majimboni mwao
kutekeleza kwa vitendo waliyoyapanga.Mkutano huo wa Tisa wa Baraza la
Wawakilishi umeahirishwa leo June 23 hadi Jumatano ya Septemba 27, 2017.
Post a Comment