Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi. Irina
Bokova ametoa taarifa katika Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Kuenea
kwa Jangwa na Ukame Duniani, 17 Juni 2017. MO Blog imekuwekea hapa
unaweza hapa chini.
Hii lazima iwe kauli mbiu yetu leo – hasa katika mapambano dhidi ya kuenea kwa jangwa.
Mchango wa mabadiliko ya mazingira
katika uhamiaji na makazi ya watu uko wazi duniani kote. Idadi kubwa ya
‘wakimbizi wa mazingira’ sasa huwasilishwa kama moja ya matokeo makubwa
ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuenea kwa jangwa. Na hili hii
inategemewa kundelea kuongezeka. Kufikia 2030, Sekretarieti ya Umoja wa
Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa imeonya kuwa, kufikia mwaka
2030 watu wapatao milioni 135 wako katika hatari ya kuhama makazi yao
kwa sababu ya kuenea kwa jangwa, na watu milioni 60 wanatarajiwa kuhama
kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara kuelekea Afrika ya Kaskazini na
Ulaya.
Utabiri huu unaonyesha kuwa sehemu
zilizo kame na zile zilizo kame zaidi huathirika zaidi na kuenea kwa
jangwa na kuhama kwa watu. Watu wanaokaa vijijini amabao hutegemea
ufugaji wa wanyama, kilimo na maliasili watakuwa katika hatari zaidi ya
kuwa wahanga wa athari hizo, ambazo hujumuisha umaskini, kudorora kwa
elimu, ukosefu wa uwekezaji, umbali kutoka huduma muhimu, na kutengwa.
Ni lazima tukabiliane na hali hii na hii inamaanisha kufanya kazi katika ngazi mbili:
Kwanza, ni lazima tusimamie ardhi
kwa usahihi,hii ni muhimu katika kuzuia kuenea kwa jangwa na katika
kulinda kiwango chake cha uzalishaji. Hifadhi ya Bayongahewa ya Las
Bardenas Reales ya UNESCO iliyoko nchini Hispania inaonyesha kwamba
usimamizi wa ardhi kame unaotumia taarifa sahihi, kwa kuzingatia
kupishana kati ya matumizi ya malisho, ukulima na vipindi ya bila ya
kuilima ardhi hupelekea si tu kusitisha kuwepo hali ya kuenea kwa jangwa
lakini pia huleta uwezekano wa kurejesha ardhi kama ilivyokua awali.
Hii ndio sababu Programu ya Kimataifa ya UNESCO ya Nishati-Maji
imejikita katika kujenga uwezo na kutoa mwongozo wa sera na zana za
kushughulikia ukame, kuenea kw jangwa na changamoto zinazotikana na
hayo, hasa kuhusiana na usimamizi wa rasilimali maji, kwa njia ya
Mtandao wa Kimataifa unaohusika na Maji na Maendeleo ya Taarifa ya Ardhi
Kame (G- WADI).
Pili, inatupasa kuimarisha
ustahimilivu wa watu walio katika mazingira hatarishi kwa kuwawezesha
kuwa na njia mbadala za kujipatia kipato ili tuweze kuuharibu mduara wa
kuenea kwa jangwa na madhara yake ya kijamii na kiuchumi ambayo mara
nyingi husababisha watu kuyahama makazi yao. Katika kutafuta na
kuendeleza elimu na kujenga uwezo katika sayansi, teknolojia na
uhandisi, kwa wasichana na wavulana katika nchi zilizo katika hatari
zaidi, Programu ya Sayansi ya Msingi ya Kimataifa ya UNESCO inafanya
kazi ya kujenga fursa mpya za ajira kwa vijana, kupunguza utegemezi wa
rasilimali zinazotegema hali ya hewa, ili kuwapatia watu maisha yenye
ustahimivu katika makazi yao.
Katika siku hii, ni lazima tutambue
kuwa hali ya kuenea kwa jangwa ni jambo la kimataifa ambalo
linalomtishia kila mtu na ni lazima lishughulikiwe kwa pamoja ili
kujenga mustakabali endelevu na imara kwa wote.
Post a Comment