Na Jonas Kamaleki-MAELEZO
Mkazi wa Mkoa wa Iringa, Thomas
Lubinza ametembea zaidi ya kilometa 502 kumuunga mkono Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zote
anazozifanya katika kulinda na kusimamia raslimali za watanzania.
Akizungumza na waandishi wa
habari, Lubinza amasema kuwa Rais Magufuli kwa kipindi kifupi cha
uongozi wake ameweza kufanya mambo makubwa ikiwemo kudhibiti na
kupambana na vitendo vya rushwa, kurudisha nidhamu serikalini na
kuboresha miundombinu.
Licha ya juhudi hizi zinazofanywa
na Mhe. Magufuli,wapo ambao wanabeza jitihada hizi na wengine kukejeli,
alisema Lubinza na kuongeza kuwa yeye ameona ni vyema ajitokeze
kumpongeza.
“Tunafahamu fika kuwa lengo la
watu wengine ni kumvunja moyo Mheshimiwa Rais ili aachane na vita hiyo
ya kupambana na maovu, mimi pamoja na watanzania wengine wenye nia njema
na nchi hii bila ya kujali tofauti zetu za kisiasa, kikabila, kidini
hata kikanda tumeamua kuunga mkono waziwazi kwa hatua zinazochukuliwa na
Serikali yetu”, alisisitiza Lubinza.
Aidha, Lubinza amewaomba
watanzania wote wamuunge mkono Mhe. Rais Magufuli kwani nia yake ni
njema ya kuibadilisha Tanzania na kuifanya nchi yenye uchumi mzuri wa
viwanda.
Ameongeza kuwa ameamua kufanya
matembezi ya hiari ili kujionea kero za wananchi wakati akiwa njiani
kuelekea Dar es Salaam. Ametaja baadhi ye kero hizo kuwa ni ukosefu wa
maji, masoko ya kuuzia mazao ya wakulima, na madereva kutokuwa na
mikataba mizuri.
Lubinza amesema licha ya
changamoto hizo, Serikali ya Awamu ya Tano imejitahidi kutatua
changamoto nyingi hapa nchini ikiwemo migogoro ya ardhi, kuboresha elimu
na kuitoa bure, kuimarisha sekta ya afya na kuboresha usafiri na
usafirishaji.
Safari hii alianza Juni 17, 2017
akitokea Iringa mjini kuelekea jijini Dar es Salaam, ambapo aliwasili
Juni 26 ikiwa ni takriban siku tisa.
Rais John Pombe Magufuli ameungwa
mkono na makundi ya watu mbali mbali ndani na nje ya nchi. Uungwaji
mkono huu umeshika kasi hasa baada ya kuzuia mchanga wa madini
kusafirishwa nje ya nchi na kuunda tume mbili kuchunguza aina na thamani
ya madini yanayopatikana katika mchanga huo. Tume hizo zikiongozwa na
maprofesa zilitoa matokeo ambayo yaliwasimumua watanzania na watu
wengine nje ya nchi.
Ameungwa mkono na wasomi wa vyuo
vikuu, vijana wazalendo, viongozi wa dini na na wananchi wa kawaida.
Hakika juhudi zake Rais Magufuli kurekebisha Taifa zimekuwa dhahiri.
Post a Comment