baadhi
ya Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mh. Simbachawene, W-OR-TAMISEMI,
wakionekana wenye furaha wakati wa Uzinduzi wa UMITASHUMTA 2017.
Ni baadhi ya Maafisa elimu kutoka mikoa mbalimbali nchini wakishuhudia Uzinduzi wa michezo ya 22 ya UMITASHUMTA Jijini Mwanza
Timu ya UMITASHUMTA ya mkoa wa Arusha, wakiwa wametangulia na mabango wakati wa Uzinduzi wa mashindano hayo.
.
Mh.
George Simbachawene, akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza
Projestus Rubanzibwa alipofika kufungua rasmi Mashindano hayo.
Katibu mkuu Baraza la michezo la Taifa Mohamed Kiganja akipeana mkono na Mh. Waziri. OR-TAMISEMI.
Mhe.
Waziri akisalimiana na Mchezaji wa timu ya waschana ya Kigoma
aliyeonekana kuwa mdogo, mara baada yakufungua Mashindano hayo, (Picha
zote na Afisa Habari Mwanza RS).
……………………….
Na Atley Kuni- Mwanza
Serikali imesema ni marufuku kwa
shule ambayo itakuwa haina viwanja vya michezo kupatiwa kibali cha
kufungua shule ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka
1978.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi
wa Masindano ya kwashule za msingi nchini UMITASHUMTA mkoani Mwanza,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMO) Mh. George Simbachawene, amemuagiza Kamishna wa Elimu
nchini, kutozipatia vibali shule zinazo hitaji kufunguliwa endapo
zitakuwa hazina viwanja vya michezo.
Simbachawene, amesema kutokana
na sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978, ambayo inataka kila shule
inapofunguliwa lazima iwe na viwanja visivyo pungua vitano hivyo
nilazima hili lizingatiwe, “nichukue nafasi hii kumuagiza kamishna wa
Elimu kuanzia sasa asisajili shule yeyote ile ambayo itakuwa haina
Viwanja vya michezo, kwani bila kufanya hivyo azma yetu yakuinua michezo
nchini haiwezi kutimia” alisema.
Mbali na kutoa maagizo hayo
waziri Simbachawene, ameziagiza pia halmashauri na wilaya kote nchini
kutenga sehemu ya mapato yao ya ndani kwaajili ya kitengo cha michezo,
huku akizihimiza kuweka katika bajeti ijayo ya serikali fedha kwenye
vifungu vinavyo husiana na michezo na kuonya kuwa endapo Halmashauri
itashindwa kufanya hivyo basi yeye kama waziri mwenye dhamana hatakubali
ipite.
Amesema Ilani ya Chama cha
Mapinduzi ya mwaka 2015 sehemu ya (61) inatambua suala la Michezo lakini
pia Sera ya Elimu ya Mwaka 1995, hivyo kama Serikali lazima waweke
kipaumbele katika suala zima la michezo.
Ameongeza kuwa, Msingi wa
Michezo nchini ni michezo ya UMITASHUMTA NA UMISETA ndio Dira ya timu
zetu za Taifa, “Tukiwaandaa vijana wetu vizuri na kutokana kaulimbiu hii
ya masula ya viwanda, hatuna wasiwasi kuwa hawa ndio viwanda vyenyewe,
mchezaji mmoja aliyefikia viwango vya kimataifa huweza kugharamia hata
bajeti ya nchi” alisema Simbachawene.
Katika hatua nyingine
Simbachawene, amewaagiza makatibu Tawala kote nchini, kusimamia suala la
taaluma na michezo, amesema hakuna taaluma bila Michezo na Hakuna
michezo bila Taaluma kwa mantiki hiyo lazima nidhamu ya hali ya juu
iongezwe miongoni mwa vijana na wanamichezo kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa Michezo
nchini kutoka Wizara ya Habari, Michezo Sanaa na Wasanii Dkt. Yusuph
Singo amesema Tayari Wadau Mbali mbali wa Michezo wakiongozwa na Chama
cha Mpira wa Miguu na Riadha wapo Mkoani Mwanza kwaajili ya Kuangalia
Vipaji kwa ajili ya Timu mbali mbali za Taifa lakini pia vilabu vyao.
Aidha amesema kuwa wizara ipo
katika Mazungumzo na Timu Manchester City kupitia wakala wao wa TECHNO
kwaajili yakuchukuwa Vijana wapatao kumi kutoka Tanzania kwaajili
yakuwaendeleza kimichezo.
Awali akimkaribisha Mgeni
rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, aliishukuru serikali
kwakuichagua Mwanza kuwa mwenyeji wa mashindano hayo huku akiomba kwa
mwaka ujao mashindano hayo kufanyika tena mkoani humo, kutokana na
madhari mazuri lakini pia ubora wa viwanja na hali ya ulinzi na usalama
inayotamalaki katika mkoa huo, “Mh. Waziri mimi niombe tu, haya
mashindando katika mwaka ujao myalete tena Mwanza sisi tupo tayari, huo
ndio mtazamo wangu lakini pia wenzangu wataniunga mkono” alisema
Mongella.
Mashindano ya shule za msingi
(UMITASHUMTA) ya 2017 ni mashindano ya 22 ambapo yanashirikisha
wanamichezo wapatao 2522 kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara.
Post a Comment