Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akimsalimia Meneja Mradi wa
kushawishi Siasa Shirikishi katika kuimarisha vyama vya Siasa hapa
nchini, hasa katika ushiriki wa Wanawake na Vijana katika masuala ya
Siasa, unaoendeshwa na Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi
(NIMD) kwa kushirikiana na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Arjan
Van Der Waal, wakati alipokutana na ujumbe wa Meneja huyo na Mwakilishi
wa NIMD Kanda ya Afrika Dk. Augustine Magolowondo (kulia), katika Ofisi
Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Watatu
kulia ni Mwenyeji wa ugeni huo, Daniel Loyc kutoka TCD.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akimsalimia Mwakilishi wa
Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) Kanda ya Afrika
Dk. Augustine Magolowondo kutoka Malawi, alipopokea na kufanya
mazungumzo na ugeni huo kutoka NIMD, leo
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akiwakaribisha kuketi kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akizungumza na ujumbea
kutoka Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) katika
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo.
Katika Mazungumzo hayo, Polepole aliitaka NIMD kuja kufanya kazi nchini
kwa lengo la kuinua hadhi ya siasa nchini badala ya kubomoa.
“Hatutarajii NIMD ije kufanya mambo hasi, mradi usilenge kuondoa
madarakani Chama tawala, bali uwe chachu katika kuhamasisha uungaji
mkono mambo mazuri yanayofanywa na Rais Dk. John Magufuli kama haya ya
kulinda rasilimali za nchi”, alisema Polepole. MAELEZO/PICHA NA BASHIR
NKOROMO
Post a Comment