MWENYEKITI wa chama cha waandishi
wa habari wanawake mkoani Pwani,(PWMO),Mwamvua Mwinyi,akizungumza katika
mkutano ulioandaliwa na halmashauri ya Chalinze na chama
hicho,uliolenga kutoa sauti ya pamoja kukemea vitendo vya unyanyasaji
kwa watoto.
MTOTO mwenye ulemavu Ibrahim
Ramadhani ,alietelekezwa na mama yake mzazi akiwa na miezi tisa ambapo
kwasasa akisoma shule ya msingi Miono,akitoa ushuhuda baada ya kusaidiwa
kibaiskeli cha kutembelea,katika mkutano ulioandaliwa
na halmashauri hiyo,na chama cha waandishi wa habari wanawake mkoani
Pwani (PWMO),uliolenga kuzungumzia masuala ya ulinzi na haki za watoto .
Mwenyekiti wa halamashauri ya
Chalinze ,Saidi Zikatimu mwenye kibagharashia akiongea na mtoto mwenye
ulemavu Ibrahim Ramadhani ,alietelekezwa na mama yake mzazi na sasa
akisoma shule ya msingi Miono,katika mkutano ulioandaliwa na halmashauri
hiyo,na chama cha waandishi wa habari wanawake mkoani Pwani
(PWMO),uliolenga kuzungumzia masuala ya ulinzi na haki za watoto .
…………………
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
WAZAZI,walezi na jamii kijumla
,imetakiwa kujenga upendo kwa watoto wenye ulemavu pasipo kuwatelekeza
ama kuwanyanyapaa, hali inayosababisha kuwakosesha haki zao za msingi
ikiwemo elimu.
Aidha halmashauri ya Chalinze
imeombwa ,kutenga fedha kwa ajili ya kuwezesha watoto wenye ulemavu
pamoja kuweka miundombinu rafiki katika katika shule za msingi na
sekondari zinazojengwa.
Mratibu kituo cha walimu ,kata ya
Miono Christopher Rutuku ,alisema hayo katika mkutano ulioandaliwa na
halmashauri hiyo,na chama cha waandishi wa habari wanawake mkoani Pwani
(PWMO),uliolenga kuzungumzia masuala ya ulinzi na haki za watoto .
Alisema wapo baadhi ya wazazi wanaowakimbia watoto wao wenye ulemavu,kutokana na kuona aibu ndani ya jamii.
Alieleza kwamba ,yupo mtoto mwenye
ulemavu wa miguu na mikono ambae ,anasoma na kuishi kwenye mazingira
hatarishi ,Ibrahim Ramadhani ,amekimbiwa na mama yake mzazi.
Rutuku alisema ,mtoto huyo
alikatishwa kunyonya na mama yake,,Moshi Musini Hamisi,wakati akiwa na
miezi tisa hivyo kuanza kulelewa na bibi yake Asha Mbegu.
“Alipoachishwa ziwa alibakia na
baba yake mzazi lakini muda mfupi kutokana na kuathirika kisaikolojia
kisa kuzaa mtoto mwenye ulemavu na kugombana na mkewe nae alipata uchizi
na kushindwa kuendelea kulea mtoto”
“Bibi yake alilazimika kuuza
shamba lake lililopo Msata akahamia Miono kwa kuwa hana mlezi ,kwasa
nafanya jitihada ya kumtafutia shule kwakuwa shule hii ya msingi
anayosoma hapa Miono haina miondombinu mizuri.”alisema Rutuku.
Rutuku ,kwasasa ameamua kuchukua
hatua ya kutafuta shule inayojihusisha kusaidia watoto wenye
ulemavu,(kituo cha Amani- Morogoro )ambapo itamsaidia kwenda kusoma
katika mazingira rafiki na bora .
Hata hivyo alisema inatakiwa kiasi
cha sh.700,000 ili aweze kuchukuliwa na kituo hicho ambapo yeye hana
uwezo wa kumpeleka hivyo anaomba msaada kwa wadau mbalimbali.
“Mnamuona huyu mtoto alivyo hawezi
kutembea anasota na mikono ikiwa ina tatizo,mtoto wa wenzio ndio wako
tusaidie namna ya kupata fedha hizo ili aweze kupata haki yake ya msingi
ya elimu”alisisitiza.
Nae mwakilishi kutoka TAMWA,Penzi
Nyamungumi,alisema watoto wote wana haki ya kupata haki zao bila
kuwagawa kijinsia ama kwa ulemavu wao.
Alikishukuru chama cha waandishi
wa habari wanawake mkoani Pwani,kwa kuona umuhimu wa kutoa sauti moja na
halmashauri ya Chalinze,kuhakikisha jamii na vyombo na taasisi
mbalimbali zinakumbushwa wajibu wao wa kusimamia masuala hayo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
halmashauri ya Chalinze,Saidi Zikatimu,akizungumzia tukio la mtoto
huyo,wataangalia uwezekano wa kusaidia kiasi hicho cha fedha .
Aliwataka wenye mamlaka katika
kutoa haki kwa watoto kuimarisha utoaji wa haki za watoto kwa
kuhakikisha wanaohusika na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia
wanachukuliwa hatua.
Zikatimu alibainisha halmashauri
hiyo inawalipia bima ya afya wazee 8 kwa kila kijiji,watoto wenye
ulemavu 8 na wanaoishi kwenye mazingira magumu wanne.
Afisa maendeleo ya jamii
halmashauri ya Chalinze Frank Makala,alisema, wanafunzi 19 wa shule za
msingi na sekondari kwenye halmashauri hiyo wamekatishwa masomo baada ya
kupata mimba katika kipindi cha mwaka 2016/2017.
“Watu waliohusika na kuwapa mimba
wanafunzi hao kesi zao ziko kwenye hatua mbalimbali za kisheria ili
hatua ziweze kuchukuliwa kwani vitendo hivyo ni kinyume cha sheria,”
alisema Makala.
Alisema kuwa kati ya wanafunzi
waliopewa mimba katika kipindi hicho wa sekondari ni 15 na wa shule za
msingi ni wanne ambao wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na kupata
ujauzito.
Mwenyekiti wa Chama Cha waandishi
wa habari wanawake mkoani Pwani,Mwamvua Mwinyi,alivitaka vyombo vya
sheria,dawati la jinsia,watendaji wa vijiji na vitongoji kila mmoja
kutimiza wajibu wake.
Alisema mimba za utotoni ,kulawiti
na kubaka ni wimbi linaloendelea kukua hivyo pasipo jitihada hali
itazidi wakati wahusika wakiendelea kutamba mitaani.
Mwamvua alitoa rai kwa waaandishi
wa habari mkoa na taifa kijumla kutumia kalamu zao kutetea haki za
watoto na wanawake ili kuwakomboa.
Post a Comment