Na Masanja Mabula –Pemba …
SUALA la bandari bubu ni moja ya agenda ilizotawala mkutano wa nne wa wakuu wa Mikoa iliyo katika mwambao wa bahari ya Hindi ya Tanzania Bara na Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mkoa wa Kaskazini Pemba .
Wakuu
hao wa Mikoa wamesema bandari hizo ndizo ambazo zinatumika kupitisha
madawa ya kulevya , magendo ya karafuu na mafuta , uingiaji wa wahamiaji
haramu ndani ya nchi pamoja na kusafirisha abiria na mizigo jambo
ambalo linapoteza mapato ya Serikali .
Akifungua
mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman ameitaja
mikoa ya Pemba pamoja na Tanga ndiyo inayoathirika zaidi na bandari
hizo kwani asilimia kubwa hutumika katika kupitisha dawa za kulevya na wahamiaji haramu .
Amesema kuwa matukio mengi ya kupotea kwa raia wa Somalia wanaokotwa katika Wilaya ya Micheweni Mkoani hapa na kushangaa kuona wasomali hao wakipotea hupotelea katika Mkoa wa Kaskazini Pemba jambo ambalo linahitaji kuchukuliwa hatua za haraka ili lidhibitiwe.
“Maeneo
ya mikoa yetu kwa kweli yako hatarini kutokana na kuwa wazi jambo
ambalo linasababisha madawa ha kulevya kupitishwa , magendo kusafirishwa
pamoja na kuingia wahamiaji haramu , wakati umefika wa kuimarisha
ulinzi katika maeneo ya bandari bubu ”alisema.
Ameeleza
kwamba katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kuna bandari Bubu 162 kati ya
hizo 88 ziko Wilaya ya Wete na 74 ziko Wilaya ya Micheweni , ambazo asilimia kubwa zinatumika kuptishia vitu ambavyo vinahatarisha usalama wa maisha ya wananchi na mali zao .
Akitoa
taarifa ya Bandari bubu , Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama ZMA Msilimiwa
Idd Msilimiwa amesema kisiwa cha Pemba pekee kina jumla ya bandari bubu
479 wakati m ikoa ya Tanzania Bara ikiwemo Tanga , Pwani , Dar es
Salaam , Lindi na Mtwara kuna bandari bubu 99.
Amesema
kwa mikoa ya Tanzania Bara Mkoa wa Pwani unaongoza kwa kuwa na bandari
Bubu 35 ukifuatiwa na Mkoa wa Tanga wenye bandari bubu 32 , Dar es
Salaam na Mtwara kila mmoja auna bandari bubu 8 na mkoa wa Lindi una
bandari 16.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Engineer Evasrto Ndikiro amezitaka SUMATRA pamoja na TPA kuitupia jicho la pekee bandari ya Bagamoyo kwani ni bandari ambayo inaweza kuingizia serikali fedha za kutosha .
Amesema
Bandari ya Bagamoyo inauwezo wa kuingiza shilingi bilioni moja kwa
mwezi , fedha ambazo kama kungekuwa na udhibiti mzuri kutoka mamlaka
husika zingeweza kutumika katika masuala mbali mbali ya kijamii .
“Bandari
ya Bagamoyo inauwezo wa kuingiza shilingi bilioni moja kwa mwezi ,
lakini fedha hizi zinashindwa kuingia kwenye mifuko ya Serikali kutokana
na kukosekana kwa udhibiti mzuri wa mapato katika bandari hiyo
”alieleza.
Hivyo
amewashauri viongozi wa Mkutano huo kuangalia uwezekano wa kununua boti
ya mwendo kasi ambayo itakuwa inafanya doria za mara kwa mara katika
mwambao wa bahari ya hindi ili kudhibiti vitendo vya uhalifu .
Post a Comment