KIKOSI KAZI CHA KUNUSURU MTO RUAHA CHAINGIA SIKU YA TATU MKOANI MBEYA.
Kikosi
kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha kilichoko mkoani
Mbeya kimeingia siku ya tatu kwa kutembelea sehemu mbalimbali na kufanya
mahojiano na Wananchi na pia kutembelea maeneo ambayo ni chanzo cha
uharibifu wa maji ya mto Ruaha mkuu pamoja na mazingira.
Katika siku ya tatu kikosi kazi
kimekutana na changamoto mbalimbali ikiwemo Wananchi kutokua na elimu ya
matumizi ya maji ya mito ambapo wengi wao hutumia pampu kutoa maji
kwenye mito ili kupeleka maji kwenye mashamba yao pasipo wao kujua kuwa
ni kosa. Mashamba mengi wilayani Mbalari yanatumia kilimo cha pampu kwa
kuvuta maji toka kwenye mikondo ya mto Ruaha Mkuu na kupeleka
mashambani. Wakulima wa vitunguu, mahindi, mpunga, nyanya, mbogamboga na
matunda.
Hutumia umwagiliaji wa aina hiyo. Pia hufanya ufyatuzi wa matofali kwa
kutumia maji yaliyoko mtoni kwa kuyavuta kwa kutumia pampu. Wakiongea
Wananchi wengi wamesema kuwa walikua hawajui kama.kufanya hivyo ni kosa
kwa sababu hawana elimu ya kutosha katika hilo.
Wengi wanalima pembezoni mwa mito bila
kuzingatia sheria ya mazingira isemayo Mkulima anatakiwa alime nje ya
mita sitini kutoka mtoni. Kikosi kazi bado kipo katika ziara yake
Mkoani mbeya katika wilaya ya Mbalari. Kikosi kazi hiki kiliundwa na
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania.
Post a Comment