KOREA kaskazini inaluamiwa kwa kuonyesha silaha bandia katika maonyesho ya hivi majuzi ya ubabe wake wa kijeshi.
Afisa wa zamani wa masuala ya ujasusi anasemna baadhi ya bunduki na makombora yaliyotumiwa kwenye maonyesho hayo yalikuw bandia.
Michael Pregent alikiambia kituo cha runinga cha Fox kuwa baadhi ya bunduki zilizokuwa kwenye maonyesho hayo zilikuwa ni za kujekesha.
Lakini maonyesho kama hayo kuonyesha ubabe wa kijeshi yametumiwa kwa miongo kadha.
Kwa sasa msukosuko ni mkubwa kati ya Marekani na Korea Kaskazini ambapo hali hiyo ni baada ya rais wa Marekani kuapa kuwa ni lazima atakabiliana na tisho la Korea Kaskazini.
"Sio kuwa Korea kaskazini inafikiri kuwa itashinda Marekani lakini kile itafanya ikiwa itashambuliwa," bwa Pregent alisema.
Historia ya silaha bandia
Silaha hizi bandia zilitengenezwa kukwepa mashambulizi ya angani na kuwachanganya marubani ya jeshi kushambulia vifaru bandia baada ya vifaru halali
Wasani ya jeshi la Ufaransa nao walichora mito bandia na mitaro ili kuwachanganya marubani wa ndege za vita.
Ujanja kama huo pia ulitumiwa wakati wa vita vya pili vya Dunia
Miongo kadha kabla miti ilitumika kupigana katika vita vya wenyewe nchini Marekani
Miti hii ilipakwa rangi hadi kifanana na silaha ya kurusha makombora.
Lengo lilikuwa ni kuwachanganya maadui kuhusu ni wapi kulikuwa na adui.
Aina hii ya silaha bandia zilitumika karne za 18 na 19
Picha hii inaonyesha wanajeshi wa Ujerumani wakikimbia ndani ya vifaru bandia miaka ya 1920
Post a Comment