Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

DC Lindi aunda kamati ya watu saba kwa ajili ya malipo ya fidia ya wananchi 106


Displaying IMG_20170422_123431.jpg
MBUNGE wa Jimbo la Mchinga mkoani Lindi Hamidu Bobali akisisitiza jambo mbele ya wananchi
Displaying IMG_20170422_123448.jpg
MBUNGE wa Jimbo la Mchinga mkoani Lindi Hamidu Bobali akizungumza na wananchi 106 wa Kijiji cha Kilangala B kata ya Kilangala ambao wanadai fidia ya kuunguliwa na mimea yao katika mashamba yao wakati wa mradi wa kupitisha bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam. Kulia ni DIWANI viti maalum CUF Somoe Hassan,Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akifutiwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mohamed Ng'aka (Picha na MPIGA PICHA wetu).

Displaying IMG_20170422_123510.jpg
Na Mwandi wetu, Lindi


MKUU wa Wilaya Lindi, Shaibu Ndemanga ameunda Kamati ya watu saba ambayo itashughulikia malipo ya fidia ya wananchi wa kijiji cha Kilangala B kata Kilangala jimbo la Mchinga mkoa wa Lindi ambao wamekuwa wakidai kwa zaidi ya miaka minne sasa.

Ndemanga aliyasema hayo jana alipokutana na wadai 106 katika mkutano uliofanyika kwenye ofisi ya kijiji cha Kilangala ambapo Mbunge wa Jimbo la Mchinga Hamidu Bobali alishiriki.

Alisema amepokea malalamiko ya wananchi wa kijiji hicho tangu alipohamishiwa wilaya hiyo hivyo ameamua kuunda kamati ambayo itashirikisha sekta mbalimbali.

Mkuu huyo wa wilaya alitaja baadhi wajumbe wa kamati hiyo kuwa wanatoka ofisi yake, usalama wa taifa, polisi, TAKUKURU, idara ya ardhi, TPDC, wananchi  na serikali ya kijiji.

Alisema kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa wiki moja hivyo kuwataka wananchi kusema ukweli ili kamati ipate urahisi wa kufikia muafaka.

"Leo ni mara ya kwanza kuja hapa na kilichonileta ni kuwaeleza ni hatua gani tumefikia kuhusu madai yenu ya mashamba kuungua tumeamua kuunda kamati ya watu saba itafanya kazi kwa wiki naomba muipe ushirikiano ili suala hili liishe," alisema.

Ndemanga alisema kuchelewa kwa malipo hayo kunatokana na kutokuwepo kwa taarifa rasmi katika ofisi yake hivyo amaamini kupitia mchakato huu mpya kila kitu kitapata muafaka.

Kwa upande wake Mbunge Bobali alisema matarajio yake ni kuona suala hilo linafikia muafaka kabla ya mwisho wa mwaka huku akisisitiza ukweli pekee ndio utaweza kusaidia.

Bobali alisema katika uongozi uliopo kwa sasa hakuna aliyehusika na tukio hilo mwaka 2013 hivyo hakuna sababu ya kuwalaumu na kuwaahidi kuwa atapigania suala hilo hadi lipate muafaka.

"Sisi hili suala tumelipokea ila naomba isitokee mtu akatulaumu kwa.sababu hatukuwepo wakati mashamba yanaungua mimi nitapigania kwa nguvu zote haki itendeke kwa watakao toa taarifa sahihi," alisema.

Akizungumzia ugumu uliopo katika mchakato wa kulipa fidia Mwakilishi wa Shirika la Petroli Tanzania (TPDC), Rodirick Mushi alisema ni kukosekana nyaraka sahihi kwa wakati huo.

Mushi alisema ushirikiano baina ya wadai na kamati ndio utarahisisha mchakato na kuwa TPDC ipo tayari kulipa kwa wakati muafaka ili kuendeleza uhusiano mwema.

"Sisi hatuna shida katika kulipa fidia hiyo ila tunataka utaratibu ufuatwe na kila mstahiki atapata anachostahiki naomba muwe wakweli," alisema.

Kwa upande wake mdai fidia Mwanajuma Mzee aliwataka wananchi wenzake kusimamia ukweli ili waweze kufaidika na madai yao.

Alisema amefuatilia suala hilo kwa miaka yote minne ila kipindi hiki wanashukuru mkuu wa wilaya na mbunge kuwaunga mkono.

Martina Madengwa aliunga mkono uwepo wa kamati huku akasisitiza uadilifu katika kazi hiyo.

Mwananchi mwingine Mussa Tanga alitoa rai kwa kamati kusimamia ukweli na kuachana na propaganda za watu ambao wamekuwa wakiposha kuhusu suala hilo.@AQA
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget