Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwa akisikilia jambo wakati wa mkutano uliomalizika jana jijini Mashahad Nchini Iran , pembeni yake kulia mwenye baragashea ni Meya wa jiji la Acra Mohamed Sowah na wakwanza kushoto ni Meya wa jiji la Kamapa Elias Lukwag. |
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wapili kulia akiwa kwenye mkutano jijini Mashad Nchini Iran, wa kwanza kulia ni Meya wa Damascas Nchi Syria
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwa kwenye mkutano jijini Mashad nchini Iran |
NA MWANDISHI WETU,
Mashahad
MEYA wa Jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amekuwa gumzo
katika mkutano uliomalizika jana Jijini Mashahad Nchini Iran baada ya kusema
kwamba Tanzania haina dini ila watu wake wana dini.
Meya ambaye yupo Nchini Iran kwa ziara ya kikazi ya siku 10,
alijikuta kwenye gumzo hilo wakati akichangia mada iliyokuwa ikiendelea ndani
ya mkutano huo ambao ulimalizika jana.
Meya alisema kwamba Tanzania ni Nchi ya amani ambayo
haijawahi kuwa na ubaguzi wa rangi, dini wala kabila na kwamba kila mmoja
aliyepo ndani ya nchi hiyo anajivunia
kuwa mtanzania.
Alisema hali hiyo imekuwa ni tofauti hata katika maeneo
mengine kwani yapo mataifa ambayo hadi sasa yanajadili udini na ukabila , na
kushauri kwamba ni vema viongozi wa kila majiji kujitahidi kutumia nafasi hiyo
ili kuondoa matabaka.
“ Watanzania kuna mambo ambayo tulijiwekea tangu enzi za Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambapo ndio msingi mkuu tulionao, hakuna
ubaguzi wa dini wala rangi, jambo kama hili ni maeneo machache sana katika Nchi
zetu kuyakuta,hivyo Tanzania tunajivunia kuwa na utamaduni huu” alisema Meya
Mwita.
Alieleza kwamba “ Jumuiya za kimataifa zimekuwa zikiwatazama
waislam wote kama watu ambao si salama nakushauri kwamba haki za kibinadamu
zizingatiwe kwao kwakuwa wote tunaumbwa na Mungu mmoja” alisema Meya Mwita.
Aliongeza kwamba “ wapo watu ambao wanaitumia dini ya
kiisilamu vibaya, nakuchafua watu
wengine , lakini tunatakiwa kutambua kwamba wote hapa tumeumbwa na mungu mmoja,
sasa dini zetu zisitufanye tukashindwa kushirikiana na kuzungumza lugha moja”
alisisitiza.
Hata hivyo katika hatua nyingine Meya alisisitiza majiji
makubwa ya nchi za kiafrika yajielekeze katika kutatua changamoto za watu wake.
Aidha Meya ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha Wairan kuja kuwekeza katika
Nchi ya Tanzania sambamba katika kuendeleza fursa za kibiashara.
Hata hivyo mkutano huo umemalizika jana na kwamba Meya kesho ataelekea
jijini Tairan kwa mualiko wa Meya wa jiji hilo ambapo pamoja na mambo mengine huko
atatembelea ofisi za umma na kukutana na wadau mbali mbali kwa ajili ya
kujadili namna ya kuendesha majiji sambamba na kutatua changamoto.
Post a Comment