Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Ufundi wa Kampuni ya Tigo, Jerome Albou
(katikati), akimkabidhi moja ya kompyuta Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule
ya Sekondari Jangwani, Amon Mgongolwa (kushoto), ambao ni msaada wa
kompyuta 10 zilizotolewa jana na kampuni hiyo kwa ajili ya matumizi ya
shule, kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi,
Dorosela Rugaiyamu na Meneja Huduma za Wateja Halima Okash.
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Shule Direct, Faraja K. Nyalandu (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kuhusu shule Direct kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Dorosela Rugaiyamu na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Jangwani, Amon Mgongolwa mara baadaa ya makabidhiano ya msaada wa kompyuta 10 zilizotolewa jana na kampuni na Tigo kwa ajili ya matumizi ya shule. |
Wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani wakishuhudia makabidhiano ya msaada wa kompyuta 10 zilizotolewa jana na Tigo kwa ajili ya matumizi ya shule, |
Kampuni
inayoongoza Tanzania katika maisha ya kidijitali Tigo leo imetoa
kompyuta 10 kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani jijini Dar es
Salaam ikiwa ni kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wasichana katika
Tehama, tukio ambalo linachangia kuziba pengo la jinsia katika sekta ya
Teknolojia ya Habari na Mawasialiano (Tehama). Kauli mbiu ya mwaka huu
ni “Ongeza Upeo, Badilisha Tabia”.
Siku
ya Kimataifa ya Wasichanaktika Tehama ni mkakati wa Umoja wa Kimataifa
wa Mawasiliano ya simu (ITU) ambao unalenga kuwezesha na kuwahimiza
wasichana na wanawake vijana kuzipa nafasi ajira zilizopo katika sekta
ya teknolojia ya habari.
Akizungumza wakati wa tukio la kutoa msaada huo lililofanyikakatika Shule ya Sekondari Jangwani, Ofisa Mkuu wa Ufundina
Mawasiliano wa Tigo, Jerome Albou alisema kuwa Tigo imejikita katika
kuchangia uwezeshwaji wa wanafunzi, hususani wasichana, ili waweze
kuingia katika mtiririko wa ulimwengu katika habari na uelewa, ambapo
watajifunza, na kupanua ubunifu wao na kushirikiana na wenzao kote
duniani kupitia mikakati iliyo ndan ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano.
“Msaada
wa kompyuta hizi upo katika mkakati wa Tigo wa kusaidia kuwawezesha
wanawake na wasichana kupitia teknolojia za habari na mawasiliano,”
alisema Albou akibainisha kuwa Tigo imejikita katika kutekeleza dira ya
serikali ya kuibadilisha nchi kuwa ndani ya uchumi wa uelewa ifikapo
mwaka 2025 kupitia ukuzaji na kuwavutia wanawake kuingia katika
mafanikio makubwa ya nguvukazi anuai.
Mgeni
rasmi katika hafla hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano katika
Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano, Dorosela
Rugaiyama,aliipongeza Tigo kwa mchango huo, akisema kwamba kompyuta hizo
zitawafikisha mbali wanafunzi katika kusambaza stadi na uelewa wa
Tehama za kisasa kwa vijana, kuwawezesha kukabiliana na changamoto za
mwenendo wa mabadiliko ya habari katika jamii na duniani kwa ujumla.
Shughuli
nyingine ambazo zilifanyika katika Shule ya Sekondari Jangwani, ambayo
ni mojawapo ya vituo vya miradi ya Shule-elektroniki ya Tigo tangu
mwaka 2015, ni pamoja na uwasilishaji wa program mbalimbali za komputa
kutoka kwa wanafunzi vijana ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao
chini ya mkakati wa Kidijitali wa Waleta mabadiliko ya Tigo (Tigo
Digital Changemakers-TDC)-wakisimamiwa na washindi wa zamani wa TDC,
Carolyne Ekyarisiima, ambaye Mradi wake wa Apps and Girls unaziba
pengo katika Tehama kupitia teknolojia za kidijtali, na Faraja Nyalandu
muasisiwa Shule Direct, ambao ni ujasiriamali jamii kidijitali ambao
unatoa mada za elimu katika kusaidia kukabiliana na changamoto za uhaba
wa walimu.
Serikali
ya Tanzania inazitaka shule kufundisha masomo ya msingi ya kompyuta
lakini ni asilimia 5 tu ya shule zina kompyuta nchini kwa sasa. Umahiri
katika Tehama unabakia kuwa mbali lakini kutokana na Tigo kutoa msaada
pamoja na wadau kuchangia malengo ya mabadiliko yanaweza kuhamasisha
wadau wengine kuchangia kufikiwa wa malengo yaliyowekwa na serikali
yanayolenga katika kuziwezesha shule zaidi ya 700 na zana za Tehama
zikiwemo kompyuta.
Mradi
wa Shule-elektroniki ni moja ya miradi ya kampuni katika mikakati ya
uekezaji kijamii na kupitia mradi huu Tigo imeweza kuunganisha shule
zaidi ya 60 za serikali nchini Tanzania na intaneti ya kasi na ya
uhakika ya 4G LTE.
Post a Comment