Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imezuia wanachama wa CUF kufanya usafi
katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni kutokana na kuwepo
kwa viashiria vya uvunjifu wa amani kutokana mvutano wa makundi mawili.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Simon Sirro amesema ombi la kufanya usafi katika mazingira ya
ofisi za chama hicho, liliwasilishwa na Mbunge wa Temeke, Abdallah
Mtolea Aprili 27 mjini Dodoma.
Amesema
kutokana na sababu za kiusalama pamoja na mgogoro wa muda mrefu
unaoendelea ndani ya chama hicho, Mbunge huyo pamoja na wanachama
wengine wanashauriwa kila mmoja kufanya usafi katika eneo lake
analoishi au analofanyia kazi.
"Kitendo
hicho cha wanachama wa CUF kukusanyika kutoka katika maeneo mbalimbali
kwa kigezo cha kufanya usafi kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani na
atakayethubutu kujitokeza atachukuliwa hatua za kisheria," amesema Sirro.
Wakati
huo huo Kamanda Sirro amesema sakata la watu waliovamia mkutano wa
iongozi wa CUF wilaya ya Kinondoni na wanahabari hadi sasa
wanawashikilia watu saba akiwemo Mkurugenzi wa Mahusiano wa wa chama
hicho, Abdul Kambaya.
Amesema
upelelezi wa kesi hiyo, umefanyika vizuri na tayari jalada limefikishwa
kwa Mwanasheria wa Serikali kwa ajili ya hatua zaidi ikiwemo kufikishwa
mahakamani.
Jeshi
hilo pia limewataka wananchi waliowahi kuibiwa magari yao kujitokeza
katika Kituo cha Polisi Mbezi ili kuangalia kutokana,na kupatikana kwa
magari matano yanayodaiwa kuibiwa jijini Dar es Salaam.
Post a Comment