Kamanda wa polisi mkoani Pwani,
kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga, wa kwa kushoto akizungumza
na baadhi ya waandishi mkoani hapo. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya waandishi wa habari
mkoani Pwani, wakimsikiliza kamanda wa polisi mkoani humo, kamishna
msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga. (picha na Mwamvua Mwinyi)
…………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
MZEE Athuman
Ramadhan Njuila ,miaka 71 ,mkazi wa Mbwewe,Bagamoyo,mkoani Pwani
anashikiliwa na jeshi la polisi, kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka
Tisa, mwanafunzi wa darasa la pili.
Mzee huyo
alifanikuwa kufanya unyama huo baada ya kumrubuni mtoto huyo aingie
ndani ya nyumba yake kusikiliza muungurumo wa mashine.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga, alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alieleza mtuhumiwa alimwambia mtoto huyo aingie ndani kisha alimsukumia kitandani na kuanza kumwingilia kimwili.
Kamanda Lyanga,
alisema taarifa hizo walizipata kutoka kwa wasiri kuwa kuna mtoto wa
shule amebakwa lakini familia zao zimeanza mazungumzo ya kumalizana
kimya kimya juu ya tukio la binti yao.
“Baada ya kupata
taarifa hizo, tarehe 24 april mwaka huu, jeshi hili, tulimhoji mama
mzazi wa binti huyo ambae alikiri kutokea kwa tukio hilo “alisema.
Kamanda Lyanga,
alitoa wito kwa wananchi kuacha kutoa mazingira rafiki kwa wabakaji ili
kukomesha vitendo vya ubakaji kuanzia ngazi ya familia.
Alisema endapo
vitendo hivyo vikitokea inapaswa kutoa taarifa polisi haraka
iwezekanavyo ili muathirika wa tukio aweze kupatiwa matibabu mapema,
ikiwemo kukusanya ushahidi na mtuhumiwa kuchukuliwa hatua kwa wakati.
Kwa mujibu wa mtoto,
alifafanua kwamba,siku hiyo alifika kwenye nyumba ya babu na kumkuta
akiwa na bibi yake kisha baada ya muda bibi aliondoka na kumuacha akiwa
na babu yake ndipo alipofanyiwa kitendo hicho.
Kufuatia kutokea kwa
tukio hilo jeshi la polisi mkoani hapo, limefanikiwa kumkamata
mtuhumiwa Njuila, ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa na mtoto huyo
alipatiwa PF3 kwa ajili ya matibabu.
Katika tukio
jingine, kamanda Lyanga alieleza, mtu mmoja mwanaume, (23)ameuawa,kwa
kuchomwa moto na watu wasiofahamika kisha mabaki yake kutupwa katika
eneo la vichaka vya shirika la elimu Kibaha.
Alisema jeshi hilo
lilipokea taarifa kutoka kwa mlinzi wa shirika kuwa ameona mwili katika
vichaka vya shirika ukiwa umechomwa moto.
Jeshi hilo lilikagua eneo la tukio ambapo ilionekana kuwa mtu huyo aliuawa eneo jingine na kwenda kutupwa kwenye eneo hilo.
Marehemu
ametambuliwa na ndugu zake kuwa anaitwa Oscar Charles Swea (23),msukuma,
mkazi wa jiji la Dar es salaam na alikuwa ametoweka kwao kwa muda mrefu
kwa tuhuma za wizi.
Pia marehemu huyo
aliwahi kufungwa miaka miwili katika gereza la Segerea, uchunguzi
unaendelea ili kubaini waliohusika na kitendo hicho.
Post a Comment