SPIKA wa Bunge Job Ndugai amepokea taarifa ya Kamati ya Ulinzi, Mambo ya Nje na Usalama kuhusu uchunguzi wa tukio la mauaji ya askari polisi wanane yaliyofanywa na watu wasiojulikana katika Wilaya ya Kibiti Aprili 13, mwaka huu.
Kamati hiyo ilipewa jukumu hilo na Spika kufuatia mwongozo uliombwa na Mbunge wa Bukombe (CCM),Dotto Biteko Aprili 18, mwaka huu akitaka Bunge lijadili suala hilo, lakini Ndugai aliamua suala hilo lifanyiwe kazi na kamati na kuwasilisha taarifa kwake.
Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amelieza Bunge leo Alhamisi kuwa kamati hiyo ilikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwiguli Nchemba na kukusanya taarifa za kina kasha kuandaa taarifa ambayo imewasilishwa na Spika, naye akaiwasilisha serikalini kwa utekelezaji.
Post a Comment