JUMUIYA YA WATANZANIA WANAOSOMA BEIJING WAADHIMISHA MIAKA 53 YA MUUNGANO
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya watanzania wanaosoma Beijing Nchini Husein Mtoro (
katikati) aliyemwakilisha Balozi,aliambatana na Viongozi wote Wakuu
akiwemo Makam Mwenyekiti Khamis Ngwali,Katibu Mkuu Ndugu Remidius
Emmanuel,Naibu Katibu Mkuu Ndugu Alinanuswe Mwakiluma na Mweka Hazina
Ndugu Kulwa Gamba.Pamoja nao,Viongozi waasisi wa Umoja huo Ndugu
Suleiman Serera na Irenius Kagashe nao walishiriki sambamba na Viongozi
wastaafu wengine akiwemo Makam Mwenyekiti Mstaafu Ndugu Kassim
Jape,Katibu Mkuu Mstaafu Angelina Makoye,Mtunza Hazina Mstaafu Lusekelo
Gwassa katika maadhimisho ya muungano yaliyofanyika mapema wiki hii
kwa kushriki maonesho ya utalii na utamaduni.
Baadhi
ya watanzania wanaosoma katika chuo cha Beijing nchini China wakiwa
katika maonesho ya utamaduni na utalii kama moja ya maadhimisho ya miaka
53 ya Muungano wa Tanzania mapema wiki hii.
Wadau wakipozi kwa picha
Maonesho ya utalii na utamaduni yakiendelea Jijini Beijing
Mmoja
wa watanzania anayesoma Beijing akipamba maonesho hayo kwa bendera ya
Tanzania wakati wa maonesho ya utalii na utamaduni ikiwa ni maadhimisho
ya miaka 53 ya Mungano Hafla hizo zilifanyika mapemaa wiki hii.
Picha ya pamoja
Jumuiya
ya Wanafunzi Watanzania wanaosoma nchini China,wameadhimisha kumbukumbu
ya Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kushiriki
MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NA UTAMADUNI katika Viwanja vya Chuo
Kikuu cha Kimataifa cha Biashara na Uchumi jijini Beijing.Akizungumza
kwa niaba ya Balozi wa Tanzania nchini China Balozi MBELWA
KAIRUKI,Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,ndugu HUSSEIN MTORO aliwaasa
Watanzania hao kudumisha Amani,Mshikamano na kushiriki katika ajenda
muhimu za Taifa ikiwemo,kushiriki katika kukuza soko la Utalii kwa
kutangaza Vivutio vya asili vya nchi yetu,kuhamasisha Watalii wengi wa
kimataifa kutembelea vivutio mbali mbali vilivyopo Tanzania.Pia
Mwenyekiti alifikisha salam za Balozi Mbelwa za kuwatakia kila la heri
Wanafunzi wote walio katika hatua mbalimbali za kukamilisha Tafiti zao
kwa ajili ya kukamilisha masomo yao.
Post a Comment