Na.Alex Mathias
Baada ya kikosi cha
Yanga kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), benchi
la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu George Lwandamina raia wa
Zambia pamoja na Msaidizi wake Juma Mwambusi wameweke wazi kuwa mipango
yao ni kuhakikisha kikosi hicho kinatwaa mataji mawili msimu huu; ligi
kuu na Kombe la FA.
Yanga walitinga hatua
hiyo baada ya kuiondosha Prisons ya Mbeya kwa mabao 3-0 kwenye mchezo
wa robo fainali uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar juzi Jumamosi huku mabao
yakifungwa na washambuliaji tegemeo kwa sasa Amis Tambwe,Obrey Chirwa na
Simon Msuva.
Huku wakiwa na
matumaini ya kunyakuwa ubingwa wa Ligi kwa mara ya tatu mfululizo wakiwa
wanamechi tano huku watani zao wamebakiwa na mechi tatu na wakiwa na
pointi 59 na Yanga 56 endapo Simba watashinda michezo yote miwili
watafikisha pointi 68 huku Yanga wakihitaji kushinda mechi tatu na sare
moja hata wakifungwa mmoja watakuwa na pointi 69 ambazo haziwezi
kufikiwa na timu yoyote.
Kocha msaidizi wa
timu hiyo, Juma Mwambusi, amesema kuwa, wanataka makombe hayo kwa ajili
ya kupooza machungu waliyonayo baada ya kutolewa kwenye michuano ya
kimataifa ambako walielekeza nguvu zao msimu huu.
“Nguvu kubwa ilikuwa
ni kufanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, lakini kila kitu
kiligeuka ndoto baada ya kutolewa, hivyo akili zetu ni kuhakikisha
tunachukua makombe yaliyobakia hapa nyumbani.
Msimu huu Yanga
haukuwa mzuri kutokana na matatizo yaliyompta Mwenyekiti wao Yusuf Manji
suala ambalo limesababisha wachezaji kukosa morali ya kujituma huku
wakicheza bila kulipwa madai yao na kusababisha kufanya vibaya katika
ngazi zote za CAF kwani waliweza kutolewa na Zanaco FC kwenye michuano
ya Ligi ya Mabingwa na kuangukia kwenye kombe la Shirikisho ambapo napo
walitolewa na MC Alger na kutupwa nje ya mashindano.
“Tuna nafasi nzuri
kwenye ligi, japo Simba wapo juu yetu kwa sasa, hilo halituogopeshi sana
kwani tukishinda mechi zetu za viporo, mambo yatakuwa sawa, pia
tunataka kufanya vizuri katika FA kwa ajili ya kujihakikishia nafasi ya
kutinga michuano ya kimataifa msimu ujao,” alisema kocha huyo.
Yanga watakuwa wageni
wa Mbao FC siku ya Jumapili April 30 kucheza nusu Fainali itakayopigwa
kwenye uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kabla ya kuwavaa wapasua mbao
hao tayari watakuwa wameshajua wanaweze kukutana na nani endapo
watatinga Fainali hiyo kwani April 29,kwemye uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam vinara wa Ligi Simba watacheza na Azam FC
Post a Comment