Maonesho
ya wiki ya usalama na afya kazini yameanza leo siku ya Jumatano tarehe
26/04/2017 katika viwanja vya Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro
ambapo taasisi mbalimbali za serikali na binafsi zimepata fursa ya
kuonyesha namna zinavyozingatia masuala ya usalama na afya kazini kwa
wafanyakazi wao.
Miongoni
mwa taasisi zilizopata fursa ya kushiriki maonyesho hayo kwa mwaka huu
ni pamoja na kampuni za uchimbaji wa madini za Bulyanhulu, Buzwagi na
North Mara ambazo zinamilikiwa na kampuni ya uchimbaji ya Acacia.
Ambapo
katika maonesho hayo migodi hiyo ya imekuwa ikionesha vifaa mbalimbali
vya uokozi pamoja pamoja na mbinu zitumikazo kuhakikisha mazingira ya
usalama kwa wafanyakazi wao wawapo kazini.
Maadhimisho
ya mwaka huu ya siku ya afya na usalama mahali pa kazi yameandaliwa na
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) yakiwa na kauli mbiu ya “ Ongeza wigo wa ukusanyaji na utumiaji wa takwimu za usalama na afya” .
Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufikia kilele chake Aprili 28,2017.
Zifuatazo ni picha mbalimbali wakati wa maonesho hayo siku ya kwanza Aprili 26,2017
Banda la mgodi wa Bulyanhulu-Maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu wakiandaa kupokea wageni mbalimbali
Maandalizi yanaendelea
Maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu
Msaidizi
wa Meneja Mkuu wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Margaret Mandia
akimkaribisha Mkaguzi wa Mitambo Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa
Kazi (OSHA) kanda ya Kaskazini Boysafi Sabato katika banda la mgodi wa
Bulyanhulu
Mkaguzi
wa Mitambo Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kanda ya
Kaskazini Boysafi Sabato akifurahia jambo baada ya kufika katika banda
la mgodi wa Bulyanhulu
Afisa
Mazingira mgodi wa Bulyanhulu Florence Nyuki akimwelezea Mkaguzi wa
Mitambo Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kanda ya
Kaskazini Boysafi Sabato namna mgodi huo unavyotunza mazingira na
kuhakikisha usalama unakuwepo katika maeneo yao ya kazi
Afisa Mazingira mgodi wa Bulyanhulu Florence Nyuki akitoa ufafanuzi kwa mwananchi aliyefika katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
Afisa
uhakiki wa usalama kutoka mgodi wa Bulyanhulu Amina Mohamed akimwelezea
kuhusu masuala ya usalama mgodini kwa mmoja wa wananchi waliofika katika
banda hilo
Afisa
Mazingira mgodi wa Bulyanhulu Florence Nyuki akitoa maelezo kwa maafisa
kutoka shirika la Umeme nchini Tanzania (TANESCO) waliotembelea banda
hilo
Wananchi wakiwa katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
Afisa
rasilimali watu mgodi wa Bulyanhulu Mwanaisha Mosha akiwaelezea watalii
kuhusu DVD ya Bulyanhulu inayohusu usalama mgodini na mahusiano ya
jamii
Afisa
viwango vya usalama mgodi wa Bulyanhulu Setieli Kimaro akitoa elimu
kuhusu mambo ya usalama mgodini kwa wananchi waliotembelea banda la la
mgodi wa Bulyanhulu
Mdau kutoka Mgodi wa Williamson Diamonds Limited Gamba Isack akiangalia bango kubwa lililopo katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
Wananchi wakiwa katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
Afisa afya mgodi wa Bulyanhulu Tumaini Sylvanus akielezea kuhusu masuala ya afya mgodini
Afisa Mahusiano mgodi wa Bulyanhulu William Chungu akifurahia jambo na mwananchi aliyembelea banda la mgodi wa Bulyanhulu
Mhandisi wa uchimbaji mgodi wa Bulyanhulu Fikiri Thomas akiwaonesha wananchi namna wanavyochimba madini
Banda la mgodi wa Buzwagi- Maafisa kutoka mgodi wa Buzwagi wakijiandaa kwa ajili ya maonesho
Nje ya banda la mgodi wa Buzwagi
Mkufunzi
Idara ya Uokozi mgodi wa Buzwagi Azaeli Kitange akitoa elimu kuhusu
usalama mgodini kwa wananchi waliotembelea banda la mgodi wa Buzwagi
Maandalizi yanaendelea
Afisa
usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akiwaelezea wananchi
kuhusu namna mgodi huo unavyojitahidi kuhakikisha wafanyakazi wake
wanakuwa salama mgodini
Mwananchi akiuliza swali kwa maafisa kutoka mgodi wa Buzwagi
Mkufunzi
Idara ya Uokozi mgodi wa Buzwagi Azaeli Kitange akimwonesha mwananchi
aliyetembelea banda la mgodi huo vifaa vinavyotumika katika uokoaji
mgodini
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akitoa somo kwa wananchi waliotembelea banda la mgodi wa Buzwagi
Afisa
Usalama na afya mgodi wa Buzwagi Deogratius Nyantabano akimwelezea
mwananchi namna mgodi huo unavyojitahidi kuhakikisha wafanyakazi wake
wanakuwa salama kazini
Afisa Usalama na afya mgodi wa Buzwagi Deogratius Nyantabano akiendelea kutoa elimu kwa wananchi
Afisa
Usalama na afya mgodi wa Buzwagi Deogratius Nyantabano akieleza jambo
kwa mwananchi aliyetembelea banda la mgodi wa Buzwagi
Dkt. Ludovick Silima kutoka mgodi wa Buzwagi akitoa elimu ya usalama kwa wananchi waliotembelea banda la mgodi huo
Dkt. Ludovick Silima kutoka mgodi wa Buzwagi akielezea masuala ya afya kwa wananchi waliotembelea banda la mgodi wa Buzwagi
Wananchi wakiwa katika banda la mgodi wa Buzwagi
Banda la Mgodi wa North Mara- Maafisa kutoka mgodi wa North Mara wakijiandaa kuanza kufanya maonesho
Afisa usalama mgodi wa North Mara Samwel Nyansika akimwelezea masuala ya usalama mgodini mwananchi aliyetembelea banda hilo
Kulia ni Mratibu wa Huduma za Afya na
Matibabu mgodi wa North Mara Dkt. Robert Mazengo akiwaeleza wananchi
kuhusu masuala mbalimbali ya afya mgodini
Kiongozi wa awali Idara ya Mahusiano
mgodi wa North Mara Annamaria Baisi akitoa somo kwa wananchi
waliotembelea banda la mgodi huo
Mratibu wa Huduma za Afya na Matibabu
mgodi wa North Mara Dkt. Robert Mazengo akimwonesha mwananchi kifaa
kinachotumika kubaini ulevi kwa wafanyakazi wanaoweza kufika kazini huku
wamelewa
Afisa usalama na afya mgodi wa North
Mara Athanas Fredrick akiwaelezea masuala ya usalama mgodini wanafunzi
waliotembelea banda la mgodi huo
Mwananchi akitembelea banda na mgodi wa North Mara
Mratibu wa Huduma za Afya na Matibabu
mgodi wa North Mara Dkt. Robert Mazengo akitoa elimu kwa wanafunzi wa
shule za msingi waliotembelea katika banda hilo
Afisa Mazingira mgodi wa North Mara Sara Cyprian akimwelezea mwanannchi namna mgodi huo unavyotunza mazingira
Afisa usalama na afya mgodi wa North Mara Alfred Mwema akitoa elimu kwa mwananchi aliyetembelea banda hilo
Mratibu wa Huduma za Afya na Matibabu
mgodi wa North Mara Dkt. Robert Mazengo akimpima kilevi mmoja wa
wananchi waliotembelea banda hilo wakati akiwaelezea namna wanavyopima
wafanyakazi mgodini
Kiongozi Idara ya Mahusiano Jamii mgodi
wa North Mara Fatuma Mssumi akielezea masuala mbalimbali kuhusu mgodi
huo katika kuimarisha afya na usalama kazini.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Post a Comment