Mshiriki wa Mashindano ya
ujasiriamali kwa Vyuo vikuu, Tahani Said akipokea zawadi kutoka kwa
Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman
Hamad katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa
Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO).
Mshiriki wa Mashindano ya
ujasiriamali kwa Vyuo vikuu, Issah Eugenio ambaye mradi wake wa
Handbags made in Jeans umechukua nafasi ya mwanzo, akipokea zawadi
kutoka kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh
Suleiman Hamad katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na jumuiya ya
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO).
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Viwanda
Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad akiutubia wakati wa kufunga mashindano
yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO)
huko ZU kampasi kuu ya Tunguu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya SISI
Consultants, Mohamed Wario ambayo ni miongoni mwa wadhamini akitoa
nasaha zake kwa wanafunzi walioshiriki katika mashindano hayo
yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO)
huko ZU kampasi kuu ya Tunguu.
MLEZI Ushauri huo umetolewa na
Mlezi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar(ZU), Mhadhiri
wa Chuo hicho Juma Rashid Khamis wakati akizungumza katika uzinduzi wa
mashindano ya miradi ya Ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu
Zanzibar yaliyofanyika katika kampasi ya chuo hicho huku Tunguu, Unguja.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mashindano hayo pamoja na Viongozi wa ZANUSO na ZU pamoja na mgeni rasmi.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mashindano hayo pamoja na Viongozi wa ZANUSO na ZU pamoja na mgeni rasmi.
333
……………………………………………………………….
Na Juma Farid, Zanzibar.
SERIKALI ya Mapinduzi ya
Zanzibar imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na baadhi
ya Jumuiya za wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini zinazoonyesha nia ya
kuthamini fani ya Ujasiriamali kama chanzo mbadala cha kupunguza tatizo
la Ajira nchini.
Ahadi hiyo imetolewa na
Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad kwa Niba ya
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali Wakati
akifunga warsha ya Mashindano ya miradi ya Ujasiriamali kwa Wanafunzi wa
Vyuo Vikuu Zanzibar yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo
Kikuu Zanzibar ( ZU) huko Kampasi Kuu ya Chuo hicho Tunguu.
Amesema ubunifu ulionyeshwa na
wanafunzi hao katika uandishi, mikakati na bidhaa za miradi ya
Ujasiriamali waliyoiwasilisha katika Mashindao hayo inajenga ushawishi
kwa serikali na mashirika mengine ya kimataifa kuwaunga mkono ili
wafikie malengo yao ya kujiajiri na kuwaajiri vijana wengine wasiokuwa
na ajira.
Amesema bado wanafunzi wengi
wanaohitimu elimu ya ngazi ya vyuo vikuu nchini hawajatumia fursa
zinazopatikana katika fani ya Ujasiriamali ambayo imekuwa ikitegemewa na
mataifa mbali mbali duniani kupunguza tatizo la ajira hasa kwa vijana.
“ Nasaha zangu kwenu kabla ya
kuanzisha mradi wowote fanyeni tathimini na utafti wa kitaalamu kubaini
aina ya ujasiriamali unaotaka kufanya una maslahi gani na wateja wako
wahitaji bidhaa za aina gani sambamba na kuwa wabunifu wa kufanya miradi
isiyofanana.”, alisema Katibu huyo.
Aidha alieleza kwamba kwa niaba
ya Waziri wa Viwanda na Masoko, Balozi Amina Salum Ali serikali
itaendelea kudhamini miradi itakayoonyesha ustawi na maendeleo endelevu.
Pia katika juhudi za kuwajengea
uwezo wajasiriamali hao alieleza kwamba serikali itashawishi makampuni
na mashirika ya kimaita ya kibiashara kufanya kazi kwa karibu na jumuiya
hizo ili zipate soko la uhakika la kuuzia bidhaa zao.
Hata hivyo ametoa nasaha zake
kwa wajasiriamali hao kutengeneza bidhaa bora zitakazokubalika katika
soko la kimataifa pamoja na kujiongeza kitaaluma kupitia mafunzo mbali
mbali ya fani hiyo.
Mapema akizungumza Mlezi wa
Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar(ZU), Bw. Juma Rashid
Khamis ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo hicho aliwasihi washiriki wa
mashindao hayo kuendelea kujifunza zaidi kupitia kwa wajasiria mali
wakongwe ili wapate ujuzi wa ziada wa kukabiliana na ushindani wa bidhaa
na miradi ya ujasiriamali ndani na nje ya Zanzibar.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya
SISI Consultants, Mohamed Wario aliwataka Wasomi hao kutumia vizuri
fursa hiyo ya ujasiria mali kwa kuangazia sehemu tofauti ambazo bado
hazijatumiwa vizuri kibiashara zikiwemo Sekta ya Utalii, Uvuvi na
Ufugaji ili kuzalisha bidhaa bora zinazotokana na rasilimali hizo na
kuzishindanisha katika soko la ndani na nje ya nchi.
“ Kampuni ipo tayari
kushirikiana na nyinyi wakati wowote lakini lazima mjiongeze zaidi
kufikia lengo la kufanya miradi bora na inayoendana na mahitaji ya sasa
ili mpate mafanikio zaidi”, alisisitiza Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake mshiriki wa
mashindano hayo aliyeshindanisha mradi wa usindikaji wa bidhaa aina ya
Jam inayotumia kwa chakula cha mkate iliyotengenezwa kwa matunda ya
Maembe, Ehlam Ali Khamis alisema wazo la kutengeza bidhaa hizo ni
kutokana na kukosekana kwa matumizi mazuri ya matunda hayo hasa wakati
wa msimu wake hali inayosababisha kuharibika kwa kukosekana kwa viwanda
vya kusindika matunda hayo.
Akitoa ufafanuzi juu ya Warsha
hiyo, Mwanzilishi na Msimamizi wa Mashindano hayo Jumuiya ya
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Zanzibar ZANUSO, Mohamed Omar alifafanua
kwamba awali mchakato huo ulishirikisha jumla ya vyuo Sita na ulipopita
mchujo vikabaki vitatu ambavyo ni Zanzibar University (ZU), State
University of Zanzibar(SUZA) na Summait University.
Mashindano hayo wamepatikana
washindi saba ambao wamepewa Zawadi mbali mbali zikiwemo simu za Adroid,
lakini nafasi ya kwanza ambayo imeshikiliwa na Issah Eugenio kwa mradi
wa Handbags Made in Jeans, nafasi ya pili ni Ehlam Ali Khamis kwa mradi
wa Mango Jam na Tatu Ibrahim ahmad abdalla na Sabrina Khamis Machano wa
mradi wa Teke knowlge solutions company wote kutoka vyuo tofauti
vilivyoshiriki kwa awatua hiyo.
Post a Comment