KIKOSI cha
timu ya Simba kimeendelea kujifua kwa nguvu wakijiandaa na mchezo wa
nusu fainali dhidi ya Azam utakaofanyika mwishioni mwa wiki hii.
Jumamosi ya
April 29, ni nusu fainali ya kwanza ya kombe la Shirikisho la Azam HD
baina ya Simba na Azam itakaopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Kwa sasa Simba
wapo Morogoro wakijiandaa na mchezo huo ambapo chini ya Kocha Joseph
Omog na Jackson Mayanja kimeamua kujichimbia huko kwa ajili ya kuwapa
muda wa kupumzika wachezaji wake na kuwapa mbinu mpya mbalimbali.
Hii inakuwa ni
mechi ya ushindani mkubwa sana kwa timu hizi mbili zikikutana kwa mara
ya tatu ndani ya msimu mmoja ambapo katika michezo miwili ya awali ila
mmoja akishinda mchezo mmoja.
Kwa mujibu wa
Kiongozi wa Simba, Abbas Ally amesema kuwa wachezaji wana ari kubwa sana
na wako vizuri na wanaamini watapigana mpaka mwisho ili kupata ushindi
kwenye mchezo huo.
“Huu ni mchezo
muhimu sana kwetu, ni muhimu kupata ushindi ili tuweze kuingia fainali
ya kombe la Shirikisho na wachezaji wana ari kubwa sana ya ushindi na
wameahidi kupambana mpaka mwisho,”amesema Ally.
Mpaka sasa
Kikosi cha Simba kinakabiliwa na majeruhi wawili ambao wanatarajiwa
kuukosa mcheoz huo ambao ni Hamad Juma na Jamal Mnyate.
Post a Comment