Mwenyekiti
wa Muungano wa Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (MMPT)
Misheni ya Kijitonyama, Maines Mhama (kulia), akimkabidhi maua mgeni
rasmi wa maadhimisho ya siku ya wanawake wa kanisa hilo, Anitha Mshighati (katikati),
mara baada ya kuwasili kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Kanisa la
Pentekoste la Kituo cha Tabata Kisiwani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kushoto ni Mchungaji Ibrahim Mshighati mume wa mgeni rasmi.
Hapa ni furaha tupu wakati mgeni rasmi akisindikizwa kuingia kanisani |
Mgeni rasmi Anitha Mshighati akizungumza katika maadhimisho hayo.
Mwenyekiti
wa Muungano wa Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (MMPT)
Misheni ya Kijitonyama, Maines Mhama akizungumza kwenye maadhimisho
hayo.
Mchungaji
Kiongozi wa Kanisa la Pentekoste Kituo cha Tabata Kisiwani, John Shusho
akiwa kwenye maombi wakati wa maadhimisho hayo.
Kwaya ya Kanisa hilo Kituo cha Tabata Kisiwani ikitumbuiza
Nyimbo za kusifu zikiendelea.
Kwaya ya Tabata Kisiwani ikiimba.
Kwaya ya Kijitonyama ikiimba.
Kwaya ya Gongo la Mboto ikifanya vitu vyake
Kwaya ya Kipawa haikuwa nyuma kutoa burudani
Mwimbaji wa nyimbo za injili wa kujitegemea, Joyce Agato akiwajibika
Mwenyekiti
wa Muungano wa Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (MMPT)
Misheni ya Kijitonyama, Maines Mhama (kushoto), akiwa na wageni wake
mgeni rasmi na mumewe.
Ibada ikiendelea.
Ni kuimba nyimbo za kusifu na kucheza.
Mwenyekiti wa Wanawake Maines Mhama akitoa neno la maadhimisho hayo.
Na Dotto Mwaibale
WANAWAKE wametakiwa kuwa chachu ya kujenga amani nchini badala ya kusubiri iharibike.
Mwito huo
umetolewa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Muungano wa
Wanawake wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (MMPT) Misheni ya
Kijitonyama, Maines Mhama wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake kwa
kanisa hilo.
“Wanawake
tunapaswa kuwa wa kwanza kujenga amani ya nchi kuanzia kwenye familia
zetu kwani inapokosekana waathirika wakubwa ni sisi na watoto wetu”
alisema Mhama.
Alisema
amani inapokoseka shughuli zote haziwezi kufanyika nchini ikiwa pamoja
na kuabudu hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuitunza kwani inapopotea
gharama ya kuirudisha inakuwa kubwa.
Akiongelea
matukio yanayotokea nchini ya watu kuuana kama yaliyotokea Kibiti
mkoani Pwani kwa askari nane kuuana alisema wanadamu wanapaswa kumrudia
mungu bila kujali itikadi za dini.
“Matukio ya kuuana yaliyoibuka hivi karibuni yatakwisha kwa watu kuwa na hofu ya mungu na si vinginevyo” alisema Mhama.
Mgeni
rasmi kwenye sherehe hizo, Anitha Mshighati aliwataka wanawake kuungana
katika masuala mbalimbali na kuanzisha shughuli za ujasiriamali ili
waweze kujikomboa kiuchumi.
“Wanawake
serikali imetuwekea miundombinu mizuri ya kufanya shughuli zetu tutumie
fursa hiyo kujianzishia miradi mbalimbali ili tuweze kufanya mambo
makubwa ya kiuchumi” alisema Mshighati.
Post a Comment