Na Tiganya Vincent, RS-Tabora
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri kwa kushirikiana na Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo amesimamisha kwa muda uchimbaji wa madini
aina ya dhahabu katika machimbo ya Kitunda wilayani Sikonge ili kuepusha
maafa zaidi yasije yakatokea.
Hatua
hiyo inafuatia maafa yaliyokea hivi karibuni ambapo wachimbaji wadogo
wadogo sita walifariki baada ya kufukiwa na kifusi na mmoja kufariki kwa
kukosa hewa wakati wa uchimbaji wa dhahabu katika eneo la Kitunda
wilayani Sikonge.
Uamuzi
huo umetolewa jana wilayani Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabaora Bw,
Mwanri baada ya yeye na kwa kushirikiana na Kamati na Ulinzi na Usalama
mkoani humo kutembelea machimbo yalisababisha maafa hayo kwa ajili ya
kujionea na kasha kuwapa pole wafiwa.
Alisema kuwa yeye na
Kamati yake wameona ni vema wasimamishe kwa muda ili taratibu zote za
kuhakikisha usalama na zile Baraza la Taifa la Mazingira za mpango wa
ulinzi wa mazingira(Environmental Protection Plan) zinafuatwa kabla ya
kendelea na shughuli za uchimbaji.
Mkuu huyo wa Mkoa
alisema kuwa lengo ni kutaka Wachimbaji hao waendele kuchimba katika
hali ya usalama bila kuharatisha maisha yao na nguvu kazi ya Taifa.
Kufuatia
hatua hiyo , Bw. Mwanri aliwaagiza Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya
Kati na Magharibi Salim Salim na Afisa Madini Mkazi wa Tabora Laurent
Mayala kuhakisha kuwa umbali kutoka shimo moja la uchimbaji hadi jingine
unazingati matakwa ya Sheria na Kanuni kuliko ilivyo sasa ambapo kutoka
shimo hadi shimo ni mita 3 hali ambayo ni hatari.
Aliongeza kuwa ni vema
Ofisi hizo zikahakikisha kuwa wanawapanga wachimbaji wadogo wadogo hao
kulingana na matakwa ya kisheria na sio kuwaacha wachimbo ovyo ovyo
ambapo hivi sasa mashimo yako karibu karibu sana na hivyo kuhatarisha
maisha yao .
“Mimi
siko tayari kuona watu wengine zaidi wanafariki kwa sababu ya uchimbaji
usiozingatia matakwa ya kisheria na ambao hauna baraka za NEMC. Hivyo
kaeni chini na wamiliki wa mgodi muwapange vizuri kwa kuzingatia sheria
na bila upendeleo” aliagiza Mkuu huyo wa Mkoa.
“Serikali
ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ilishaahidi
kuwa itawashika mkono wachimbaji wadogo wadogo , lakini ni vema
tukahakikisha kuwa Mpango wa Ulinzi wa Kimazingira umezingatiwa na
kuwepo na wakaguzi watakao hakikisha kuwa taratibu za umbalimbali toka
shimo hadi shimo umezingatiwa ili kulinda usalama wao kwanza ”
anasititiza Mkuu wa Mko huyo
Alisema kuwa kuwepo
kwa madini ya dhahabu katika eneo la Kitunda ni neema , lakini neema
hiyo neema hiyo ni vema utafutaji wa neema hiyo ukazingatia taratibu
bila kusababisha maafa mengine kama yaliyotokea wiki iliyopita ambapo
watu watano walifia mgodini , mmoja alifia hospitalini na mwingine
alikufa kwa kosa hewa katika mgodi mwingine.
Aidha ,Mkuu huyo wa
Mkoa aliwaagiza Maafisa Madini kuharikisha katika ufuatiliaji wa Kibali
cha NEMC na kuandaa Mpango Kazi wa Uchimbaji Mzuri na salama ili vijana
wanaojihusisha na uchimbaji wa madini katika eneo la Kitunda wasikae
muda mrefu bila kuendelea na kazi yao ya uchimbaji madini.
Alisema kuwa vijana
hao hawana kazi nyingine wanayotegemea kujiingizia kipato zaidi ya
uchimbaji wa madini katika eneo hilo , hivyo ni vema watendaji hao kwa
kushirikiana na wamiliki wa mgodi huo kuhakikisha mambo yafanyika haraka
iwezekanavyo.
Aidha alitoa kwa
wachimbaji madini hao kukikisha kuwa sehemu ya mapato yao wayatumie
katika kuboresha maisha yao na familia zao kwa kujenga nyumba nzuri,
kuvaa vizuri kula vizuri na kulipa kodi zinatakiwa ili neema hiyo iwe na
tija kwao.
Bw. Mwanri alisema kuwa haitakuwa na maana ya kuwepo kwa neema hiyo kama watapata fedha na kuendelea kuishi maisha duni .
Naye Kamanda wa Jeshi
la Polisi Mkoani Tabora Wilbroad Mtafungwa ametoa onyo kwa baadhi ya
vijana wanaendesha vitendo viovu katika eneo hilo kama vile uvutaji
bangi, uporoaji na ubakaji kwa kisingizio cha uwepo wa madini ya dhahabu
kuacha mara mmoja la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Alisema kuwa Jeshi la
Polisi Mkoani huo ili kuimarisha ulinzi na kuhakikisha wachimbaji hao
wanaendesha shughuli zao katika mazingira rafiki, limeamua kufungua
Kituo Kidogo katika eneo hilo.
Hatua hiyo inalenga
kuwepo na ulinzi saa 24 siku zote kwa ajili kuwa tayari wakati wote
kukabiliana na uvunjivu na amani na sheria ambao unaweza kujitokeza..
Aidha ,RPC huyo pia
aliwaonya wachimbaji wadogo hao kutoenda katika machimbo wakati wote wa
zuio hadi hapo watakaporuhusiwa la sivyo watakabiliana na Askari
watakaokuwa wakilinda machimbo hayo
Katika hatu nyingine ,
Kamanda huyo ameowanya Polisi wote watakaokuwa wakilinda eneo hilo
kutojihusisha na uchimbaji madini kwani kufanya hivyo kutawasababisha
migogoro na wao wakuwa wamekiuka kiapo chao.
Eneo la mchimbo ya Kitunda linawachimbaji zaidi ya 10,000 ambao wanaendesha shughuli hizo .
Post a Comment