Timu ya soka ya taifa ya vijana
chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo imeifunga Gabon mabao 2-1
katika mchezo wa kirafiki mjini Rabat, Morocco.
Asante kwa wafungaji wa mabao hayo, Kelvin Nashon Naftali dakika ya 18 na Ibrahim Abdallah Ally dakika ya 75.
Serengeti Boys imeweka kambi ya mwezi mmoja nchini Morocco kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, zinazotarajiwa kuanza Mei 14 hadi 28, mwaka huu nchini Gabon.

Huo unakuwa mchezo wa nne wa
maandalizi kwa Serengeti kujiandaa fainali za Gabon, baada ya kuifunga
Burundi mara mbili, Machi 30 mabao 3-0 na Aprili 1 mabao 2-0, mechi zote
mbili zikipigwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, kabla ya kulazimishwa sare
ya 2-2 na Ghana ‘Black Starlets’ Aprili 3 Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Serengeti Boys itakuwa kambini mjini Rabat hadi Mei 1, mwaka huu itakapowenda Younde, Cameroon kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya wenyeji Mei 3 na 6, mwaka huu.
Mei 7 timu hiyo itakwenda Gabon ambako imepangwa kundi B pamoja na timu za Ethiopia ambao wamechukua nafasi ya Mali iliyofungiwa na FIFA, Niger na Angola, wakati Kundi A lina timu za wenyeji, Gabon, Guinea, Cameroon na Ghana.

Post a Comment