Na Mwamvua Mwinyi, Rufiji
Vitendo vya mauaji
mbalimbali huko Rufiji,mkoani Pwani, vimeendelea kutokea ambapo Hamad
Malinda, mkazi wa kijiji cha Mgomba Kaskazini, kata ya
Mgomba,Ikwiriri,ameuawa kwa kupigwa risasi,na watu wasiojulikana.
Tukio hilo ni la tano kutokea wilayani hapo ,kati ya matukio hayo watu watatu wamefariki dunia na wawili wamenusurika kifo.
Mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama wilayani Rufiji, Juma Njwayo,alisema mnamo saa
1-2 usiku, april 29 maeneo ya mashambani huko Mgomba Kaskazini kulitokea
tukio hilo.
Alieleza kuwa, alipokea taarifa hiyo saa 3 usiku siku ya tukio ,kutoka kwa kikosi maalum kilichopo wilayani hapo .
Njwayo alisema watu hao baada ya kufanya mauaji waliacha kipeperushi ambacho kitatumika kwenye upepelezi wa awali.
Alifafanua kwamba,
kwasasa kikosi maalum kipo eneo la tukio kikiendelea na kazi pamoja na
uchunguzi wa awali na mazishi yatafanyika april 30 jioni.
Hata hivyo Njwayo alisema ni changamoto kwani wakidhani mambo yametulia lakini wamekuwa wanashtukizwa .
“Ni tukio la tano ambapo huyu ni watatu anafariki na wawili walisalimika kifo. “
“Vipeperushi hawaviachi kwenye kila tukio lakini kwenye tukio hili wameacha,”
“Vipeperushi
wanavyoviacha wanachanganya watu tuuu, huwezi kusema viongozi wa kijiji,
kitongoji ama polisi wananyanyasa akina mama wajawazito ,Wanawake
,watoto na wazëe na wanadai nyumba zinachomwa moto na hakuna haki ni
suala la uongo .”
“Mambo haya hayana
ufafanuzi hauwezi kudai kwamba hakuna haki wakati sio mambo ya
ukweli,hakuna mwanamke wala mtoto anaeonewa katika wilaya hii “alisema
mkuu huyo wa wilaya.
Njwayo aliomba wananchi waendelee kuiamini serikali na vyombo vya dola kwani anaamini jitihada zinazofanyika watashinda.
Alisema vitendo vya aina hiyo vilishawahi kutokea baadhi ya maeneo ikiwemo Amboni ,Morogoro na serikali ilipambana na kushinda.
Nae mbunge wa jimbo la Rufiji, Mohammed Mchengelwa, alisema matukio hayo yanajenga hofu kwa wananchi.
Aliwataka wananchi kutulia kwani kikosi maalum kinaendelea na kazi na hali itakuwa shwari.
Kwa upande wake,
kamanda wa polisi mkoani Pwani kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo
Lyanga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Alieleza, jeshi la polisi kupitia makachero na askari polisi waliopo wilaya ya Mkuranga, Rufiji na Kibiti hawalali.
Lyanga alisema wanaendelea na mapambano masaa 24 usiku na mchana hadi kitakapoeleweka.
Mkazi wa Ikwiriri Seif Abubakar, aliomba serikali iboreshe mbinu na kuongeza nguvu ya upelelezi wake kwenye wilaya hizo tatu.
Hivi karibuni katika
tukio la mauaji lililofanyika tawi la Mparange, Ikwiriri Kaskazini,
watu hao waliacha kipeperushi kinachodai wanafanya vitendo hivyo ili
kukomesha vitendo vya manyanyaso wanavyofanyiwa wanawake, watoto na
wazee.
Matukio matano yaliyowahi kutokea Rufiji, kati ya
19 ambayo yamewahi kutokea Kibiti, Rufiji na Mkuranga ni pamoja march
28 ambapo mwenyekiti wa (CCM) tawi la Mparange na mjumbe wa serikali ya
kijiji cha Ikwiriri Kaskazini,aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwani na
watu wasiojulikana.
Jan 19,mjumbe wa serikali ya kijiji cha Nyambunda ,Oswald Mrope, aliuawa kwa kupigwa risasi.
March 1,mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda Said Mbwana aliuawa.
Octoba 24,2016 afisa mtendaji wa kijiji cha
Nyambunda Ally Milandu alipigwa risasi na kufa na novemba 6,2016
,mwenyekiti wa kitongoji cha Nyang’unda kijiji cha Nyambunda Mohammed
Thabiti alipigwa risasi akielekea kwake.
Post a Comment