Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akitoa hotuba yake wakati
wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Wakala wa Usalama na
Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya siku ya
Usalama na Afya mahali pa kazi uliofanyika Aprili 25, 2017 Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa
Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) wakimsikiliza Naibu wake Ofisi ya
Waziri Mkuu Mhe. Antony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa
waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi hiyo ikiwa ni maandalizi ya ya
maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi uliofanyika Mjini
Dodoma.
Kaimu Mtendaji Mkuu OSHA Bi.
Khadija Mwenda akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa habari juu
ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya mahali pa Kazi
uliofanyika Mjini Dodoma Aprili 25, 2017.
Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Bw.Peter Kalonga akichangia hoja wakati wa Mkutano na waandishi
wa habari juu ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya
mahali pa Kazi uliofanyika Mjini Dodoma Aprili 25, 2017.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akisalimiana na Mwakilishi
wa TUCTA Bw.Ramadhani Mwenda mara baada ya mkutano wa waandishi wa
habari Aprili, 25, 2017 Dodoma
Naibu wake Ofisi ya Waziri Mkuu
(Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde (katikati waliokaa) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Wakala wa Usalama na
Afya Mahali pa Kazi (OSHA)mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa
habari Aprili 25, 2017 Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)
………….
Na. Mwandishi Wetu- Dodoma
Serikali imewataka waajiri wote na
wadau kwa ujumla kuhakikisha kuwa sehemu za kazi, mitambo na vifaa
vya kufanyia kazi vinafanyiwa ukaguzi mara kwa mara ili kuhakikisha
kuwa havileti madhara kwa wafanyakazi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Ajira na Vijana
Mhe. Antony Mavunde wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo mjini
Dodoma kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya
mahali pa kazi.
“Kwa upande wa Serikali jukumu
letu kubwa ni kuweka na kusimamia sera ya Usalama na Afya Mahali pa
Kazi, kutunga na kusimamia Sheria za Usalama na Afya Mahali pa Kazi, na
kuweka viwango mbalimbali vya usalama na afya sehemu za kazi”
alisisitiza Mavunde.
Mavunde alisema kuwa kwa sasa
kanuni ya kuripoti ajali na magonjwa imekamilika na kuanza kutumika
tangu mwezi Septemba, mwaka 2016.
Ambapo ameshauri wafanyakazi
kuwasaidia waajiri wao kusimamia mifumo iliyopo, kujilinda wao binafsi
ili wasiumie ama wasipate magonjwa yatokanayo na kazi sambamba na
kutumia ipasavyo vifaa vyote vya kujikinga wawapo kazini.
Mavunde alisema kuwa serikali
inaendelea kuboresha mfumo wa ukusanyaji takwimu za ajali na magonjwa
yatokanayo na kazi, hivyo bado kuna changamoto ya kupata taarifa kuhusu
ajali na magonjwa yatokanayo na kazi hii inatokana na waajiri wengi
kutoripoti taarifa hizo kama sheria inavyoelekeza.
kwa mantiki hiyo Serikali inaandaa mfumo ambao utaongea na mifumo mingine ili kupata taarifa za ajali na magonjwa.
Aliongeza kuwa “Serikali kupitia
Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) imejipanga kuhakikisha
kuwa Usalama na afya za wafanyakazi hao zinalindwa kwa kuhakikisha kuwa
waajiri wanazingatia taratibu zote za Usalama na Afya kwa mujibu wa
sheria na 5 ya Mwaka 2003, ili kulinda nguvu kazi ya taifa hili”.
Aidha, tarehe 28 Aprili ya kila
mwaka, Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku
ya Usalama na Afya Mahali pa kazi ili kuwakumbuka wahanga wa majanga
yanayotokea sehemu za kazi.
Madhumuni makubwa ya kuadhimisha
siku hii ni kuendesha kampeni ya Kimataifa ya kuboresha usalama na afya
kazini na kuhamasisha utengenezaji ajira zenye staha.
Kwa kuhamasisha waajiri na
wafanyakazi na umma kwa ujumla kuchukua hatua za makusudi ili
kuhakikisha kuwa suala la ajali na magonjwa yatokanayo na kazi
yanapungua au kutotokea kabisa sehemu za kazi.
Maadhimisho ya mwaka huu
yanatarajia kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kujumuisha shughuli
hizo kuanzia tarehe 25 hadi tarehe 27 ambapo yatatanguliwa na
kongamano la wadau wa Usalama na Afya.
Post a Comment