Waziri mkuu Kassim Moajaliwa
amekutana na mabalozi wa Tanzania wanaenda kuiwakilisha Tanzania katika
nchi mbalimbali kuhakikisha wanaimarisha uhusiano na kujenga urafiki
kati ya nchi wanazowakilisha kwa lengo la kuitangaza Tanzania
kiuchumi,ikiwa ni pamoja na kueleza fursa za uwekezaji na utalii
zilizopo nchini.
Mabalozi wa Tanzania walioteuliwa
hivi karibuni na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,kuwakilisha
Tanzania nnje ya Nchi,wamefika ofisi ya waziri mkuu mjini Dodoma kwa
lengo la kumuaga na kwenda kuanza majumukumu yao katika nchi
walizopangiwa.
Waziri mkuu amewaleeza mabalozi
hao kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za uwekezaji Na jukumu lao la
kwanza la Mabalozi hao ni kuvitangaza vivutio vilivyopo ili kuleta
wawekezaji wengi TANZANIA .
Suala la ushirikishwaji sekta binafsi pia waziri mkuu amesema Tanzania imelipa kipaumbele
Waziri Mkuu alizungumzia sula la
watanzania waishio nje ya nchi , aliwataka Mabalozi kuwakutanisha na
kufanya nao mikutano mara kwa mara ilikujua kama wanamatatizo
yanayoyapata katika nchi wanazoishi ilikuangalia jinsi gani wanaweza
kusaidiwa,
Mabalozi hawa wanaenda
kuiwakilisha Tanzania katika nchi za QATAR,UBELIGIJI,AFRIKA
KUSINI,UJERUMANI,COMORO,ALGERIA,INDIA NA ,SUDAN.
Post a Comment