Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia kwenye shughuli za mazingira ambapo nyavu zilizotumika kwenye
uvuvi haramu zimeteketezwa katika dampo la Buhongwa, wilaya ya
Nyamagana mkoani Mwanza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akishiriki kuchoma nyavu za uvuvi haramu kwenye dampo la Buhongwa,
wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
ameagiza vyombo vya dola nchini kuwakamata bila kuwaonea huruma viongozi
watakaobainika kujihusisha au kuhujumu kazi ya kupambana na uvuvi
haramu nchini.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo wakati akishiriki
katika zoezi la uchomaji wa zana haramu za uvuvi 5,662 kwenye eneo la
Buhongwa wilayani Nyamagana mkoani Mwanza zilizokamatwa katika Ziwa
Victoria.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya
viongozi kushiriki katika shughuli za uvuvi haramu hivyo inabidi
wachukuliwe hatua ili kukomesha kabisa tatizo la uvuvi haramu katika
Ziwa Victoria na maeneo mengine nchini.
Ameeleza
kuwa uvuvi haramu katika Ziwa Victoria umekuwa ni tatizo sugu na hali
ambayo imesababisha kupungua kwa samaki na mapato kwa Serikali ambayo ni
muhimu kwa ajili ya shughuli maendeleo.
Amesema
licha ya uvuvi haramu kupunguza mapato ya Serikali kutoka kwenye
viwanda hali ya ajira nayo sio nzuri zilizokuwa zinatoka kwenye viwanda
ambazo zimepungua kwa asilimi 49.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepongeza kazi kubwa iliyofanyika ya
ukamataji wa zana haramu za uvuvi katika Ziwa Victoria na
amewahakikishia viongozi wa mkoa wa Mwanza kuwa Serikali ipo pamoja nao
katika kazi hiyo.
“Serikali
yenu itaendelea kushirikiana nayi katika kuhakikisha kuwa rasilimali za
uvuvi katika Ziwa Victoria zinaendelea kuwepo kwa kuendelea kutoa fedha
na vitendea kazi ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi kwa lengo
la kuhifadhi ziwa Victoria” Amesisitiza Makamu wa Rais.
Kwa
upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amesema oparesheni za
uvuvi haramu katika Ziwa Victoria zitaendelea kuimarishwa ipasavyo
mkoani Mwanza mpaka vitendo hivyo vikomeshwa.
Amesema
mkoa wa Mwanza ulikuwa na viwanda Sita vya kuchakata samaki lakini
kutokana na kupungua kwa samaki katika Ziwa Victoria ni viwanda Vinne tu
mpaka sasa ndio vinafanya kazi hali ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa
mapato kwa Serikali na ajira kwa vijana mkoani huo.
Mkuu
huyo wa Mkoa wa Mwanza John Mongela ameeleza kuwa kutokana na viwanda
hivyo kusitisha shughuli za uzalishaji zaidi ya watu mamia ya watu
wamekosa ajira.
Post a Comment