Mwanafunzi
kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Benson Mcharo
amejinyakulia zawadi ya kiasi cha Sh. Milioni 2, baada ya kuibuka
mshindi wa kinyang’anyiro cha shindano la uwekezaji kwa wanafunzi wa
vyuo vikuu na shule za sekondari nchini, lilioandaliwa na Soko la Hisa
la Dar es Salaam (DSE).
Mcharo
amekuwa mshindi upande wa wanafunzi wa vyuo vikuu, wakati Irene David
kutoka Shule ya Sekondari ya Scolastica kutoka mkoani Moshi
akijinyakulia zawadi ya milioni 1, baada ya kuibuka kidedea kwa upande
wa wanafunzi wa shule za sekondari.
Aliyekuwa
Mgeni Rasmi katika hafla ya ugawaji tuzo hizo,Katibu Mtendaji wa Baraza
la Uwekezaji Tanzania (NEEC), Beng’i Issa ameipongeza DSE kwa kuandaa
shindano hilo kwa kuwa linasaidia kutoa elimu ya masuala ya uwekezaji
kwa wanafunzi nchini.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa hundi za pesa walizozawadiwa, Mcharo amesema
hakutarajia kuwa mshindi kwani shindano hilo lilikuwa na ushindani mkali
na kwamba haikuwa jambo jepesi kuibuka kinara
“Nimefurahi
sana kushinda, lakini shindano hili halikuwa rahisi sababu nilishiriki
wakati nikiwa masomoni, na kupelekea kufanya mambo mawili kwa wakati
mmoja yenye kuhitaji utulivu wa akili,” amesema.
Naye
Irene amesema amefirahi kupokea tuzo hiyo, na kwamba ataendelea kufanya
uwekezaji kwenye soko hilo kwa ajili ya kujiingizia kipato pamoja na
kupata elimu ya ziada ya kuwa mchumi bora hapo baadae.
Aidha,
mshindi wa pili kwa upande wa vyuo vikuu ni Frank Johnson
aliyejishindia mil. 1.5 kutoa Chuo cha Ardhi, wakati wa tatu akiwa ni
Charles Msongwe (laki tano) kutoka SUA, huku nafasi ya nne ikichukuliwa
na Omega Emanuel (laki tatu)kutoka SUA.
Kwa
upande wa shule za Sekondari, nafasi ya pili ilichukuliwa na
Christopher Ngonyani (Laki 6) kutoka Kibaha Boys, wakati wa tatu akiwa
ni Emanuel Mwenda (Laki 4) kutoka Kibaha Boys.
Post a Comment