Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

May 2017


MWAI
Na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji imeanzisha dawati la wepesi wa kufanya biashara ambao lina jukumu la kuondoa ugumu wa kuanzisha na kuendesha biashara  nchini.
Hayo yamesemwa leo Bungeni na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Magomeni Mhe.Jamal Kassim Ali.
“Ujenzi wa Viwanda nchini unategemea zaidi mazingira ya uwekezaji yaliyopo ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa ardhi yenye miundombinu wezeshi,sera mbalimbali,mifumo ya kodi na mifumo ya upatikanaji wa vibali  vinavyotakiwa kisheria ambayo ni majukumu ya Serikali”Alisema Mhe.Mwijage.

unnamed
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charels Mwijage akiongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kuhudhulia kipindi cha Asubuhi cha kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba Bunge la 11 Mei 26,2017.
HAWA
Mbunge wa Mtwara Vijini (CCM) Mhe. Hawa Ghasia wakijadiliana jambo na Mbunge wa Momba (CHADEMA) Mhe. David Silinde katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma wakati wakiingia katika ukumbi wa Bunge kuhudhulia kipindi cha Asubuhi cha kikao cha 35 Mkutano wa Saba Bunge la 11 Mei 26, 2017.
MWE
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Najma Giga akiongoza kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
KAWE
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017. 
  MAJ
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge kazi Ajira Vijana na watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
  JAFO 
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.  
 LUB
Mbunge wa Mpwapwa (CCM) George Lubeleje akiuliza swali katika kikao cha 35 cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017. 
   EDW
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akijadiliana jambo na Naibu waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017. 
   unnamed
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt Medred Kalemani katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.   
MWAI
 Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
NASI
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakifurahia jambo na Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassari katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017. 
  SAKAYA
Mbunge wa Kaliua (CUF) Mhe. Magdalena Sakaya akiuliza swali katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.   
NCHEMB
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
MJAD
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
WAMBU
 Naibu waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anstazia Wambura(kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe(katikati) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt Medred Kalemani wakati wakijadiliana jambo katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.  
HAULE
Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Mhe. Joseph Haule (Kulia) pamoja na Mbunge wa Mikumi Mhe. Joseph Haule (wa pili kulia) na Mbunge wa Tunduma (CHADEMA) Mhe. Frank Mwakajoka (aliyeipa kisogo kamera) wakimsikiliza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charels Mwijage wakati wakijadiliana jambo katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
unnamed
Mbunge wa Bunda Mjini (CHADEMA) Ester Bulaya akiuliza swali katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017. 
MAJA
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Ritha Kabati katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
WAF
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Compassion English Medium kutoka mkoani Njombe wakiwa Bungeni wakifuatilia shughuli za Bunge katika dhumuni la kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Picha Zote na Raymond Mushumbusi Dodoma MAELEZO, DODOMA


Image result for picha ya malinzi




Mechi namba 206 (Yanga 1 Vs Toto Africans 0).
Klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani wakati wa mechi hiyo iliyochezwa Mei 9, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu. Uamuzi huo umezingatia pia kuwa Yanga imekuwa ikirudia kosa hilo mara kwa mara.

Mechi namba 225 (JKT Ruvu 0 Vs Majimaji 1).
Timu ya Majimaji haikuingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi hiyo iliyofanyika Mei 13, 2017 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.


SEL1
Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Bw. Lazaro Kitandu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System). Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Bw. Richard Kasuga.      
Picha na Fatma Salum- MAELEZO

DK.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitoa risala ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla na kuwatakkia kheri katika mwezi huo,pia amewataka kujitahidi kufanya ibada kwa wingi,ikiwemo kusima Quran,kuswali sana hasa swala za Suna na kutoa zaka,[Picha na Ikulu.] 26/05/2017.


Image result for picha ya meya wa jiji


 NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita , jana amezindua mashindano ya ngumi ya kombe la mstahiki Meya na kusisitiza kuwa kuna kila sababu ya kutoa kipaumbele kwenye mchezo huo ili uweze kuwa ajira sambamba na kuibua vipaji kwa vijana.
 Meya Mwita alisema kuwa michezo ni afya na kwamba atajitoa kadiri ya uwezo wake ili kufanikisha mchezo huo kuwa chanzo cha ajira kama ilivyokuwa kwenye nchi za nje.
Alifafanua kuwa nchi nyingine wapo watu walioajiriwa kupitia mchezo huo na kwamba hata hapa kwetu uwezo huo upo lakini kinachotakiwa ni kujitoa na kuthamiria kuwekeza nguvu kubwa kwenye mchezo huo.

Mwagala
Inline image 7
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita, akihutubia Umma wa kislamu  uliofika katika dua maalum ya  kumuombea  Shekhe Yahya Hussein  pamoja na kukaribisha mwezi mtukufu Ramdahani unaotarajia kuanza mwishoni mwa wiki hii. Dua hiyo ilifanyika   katika Makaburi ya Tambaza Jijini Dar es salaam janaBaadhi ya waumini wa dini ya kiislamu waliohudhuria   dua maalumu ya kuwaombea marehemu na vipenzi vya Mtume Muhamad (s.a.w) iliyofanyika jana katika makaburi ya Tambaza, Upanga Mashariki jiji Dar es Salaam
Inline image 2

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita, akiwa kwenye dua ya pamoja na baadhi ya mashehe waliohudhuria dua maalumu ya kumuombea Sheikh Yahya Hussein sambamba na kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Dua hiyo ilifanyika jana katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga Mashariki jijini hapa.

Inline image 3

Mstahiki Meya Isaya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mjukuu wa marehemu Shekhe Yahya Hussein, Yahya Hussein wakati akisoma Quruan Tukufu  katika Makaburi ya Tambaza Jijini Dar es salaam jana 

Inline image 4

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita, akipokea risala maalumu iliyoandaliwa na Taasisi ya Shekhe Yahya Hussein katika dua maalumu  ya kumuombea Shekhe Yahya Hussein pamoja na kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani  katika  makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga Mashariki Jijini Dar es salaam jana
Inline image 5
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam, Isya Mwita, akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya mashehe  waliohudhuria dua maalumu ya kumuombea Sheikh Yahya Hussein sambamba na kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani  katika makaburi  ya Tambaza  yaliyopo Ukonga Mashariki Jijini Dar es salaam.
Inline image 6


Inline image 8


Image result for picha ya anthony mavunde
Na DaudiManongi
Serikali kupitia Baraza la Uwezeshaji wana nchi kiuchumi (NEEC) lililopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imewataka wananchi kuitumia vyema mifuko 19 ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ilikujipatia mitaji yenye riba nafuu.
Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana Mhe.Anthony Mavunde wakati akijibu maswali mbalimbali ya wabunge leo Mjini Dodoma.

unnamed
Mchoraji  Nembo ya Taifa , Mzee Francis Maige Kanyasu akiwa katika Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake. Mzee Kanyasu amefikishwa leo MNH akitokea Hospitali ya Amana.
A
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni Mkuu wa Idara  hiyo  Juma Mfinanga akimuhudumia Mzee Kanyasu mara baada ya kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Dar es salaam                                                     25-05-2017
Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- imeanza kumfanyia uchunguzi mchoraji  wa Nembo ya Taifa , Mzee Francis Maige Kanyasu .

Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Dk. Juma Mfinanga amesema  Mzee Kanyasu amechukuliwa leo asubuhi kutoka Hospitali ya Amana ambako alipelekwa jana na majirani zake na kupatiwa matibabu ya awali.

unnamed
 Mwenyekiti wa Bunge Mwenyekiti   wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Najma Giga akiongoza kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
JE
Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama  akiomba Bunge kutengua Kanuni zake na kuruhusu Bunge kuhairisha shughuli zake saa kumi na mbili jioni ili kuruhusu wabunge ambao ni waumini wa dini ya Kiislaamu kutimiza matakwa ya mfungo mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza Jumamosi.
unnamed
 Naibu Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana,Ajira na Kazi Mhe. Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
OLE
 Mhe. William Ole Nasha Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
MBAAAAAAAA
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Prof Makame Mbarawa na Naibu wake Mhe.Edwin Ngonyani wakijadiliana jambo katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
LUK
 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akiwasilisha  Makadirio ya Maapto na Matumizi ya Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.

MCH
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Philip Mpango katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
MWAI
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji  Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.

unnamed
Na Jacquiline Mrisho.
Tanzania ya viwanda inayoelekea kwenye uchumi wa kati ni moja kati ya mipango mikubwa ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli katika azma yake ya kuleta Maendeleo  nchini.
Akihutubia Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya Tano, Magufuli alisema kwamba Serikali yake itaweka mkazo mkubwa katika ujenzi wa Viwanda.
“Natambua kwamba sekta binafsi ndiyo mhimili mkubwa wa kujenga uchumi wa viwanda. Tamaa yangu na kwa kweli jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano zitakuwa katika ujenzi wa uchumi wa kipato cha kati ambapo sura  na maisha ya Watanzania walio wengi yafanane na nchi za kipato cha kati” alisema Rais Magufuli.


unnamed
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wakati wa ibada Maalum ya kuliombea Taifa la Kenya iliyoandaliwa na Bunge la nchi hiyo. Wengine katika  pichani kutoka kushoto ni Spika wa Bunge la Kenya  Justin Muturi, Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe  Ekwee Ethuro na Jaji Mkuu wa Kenya Jaji David Maraga. Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la Kenya ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge, Mhe Mary Chatanda, Mhe Salim Turky na Mhe Mch.Peter Msigwa.

Na Zainab Nyamka


Kiungo mahiri wa timu ya Mbeya City Kenny  Ally amejiunga rasmi na klabu ya Singida United kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa kandarasi ya miaka miwili.


Kenny ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wakiwindwa vikali na klabu kubwa za hapa nchini Simba na Yanga kila mmoja akitaka kupata saini yake ila walikuwa wakishindwana katika dau.



  Naibu Waziri,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt.Hamisi Kigwangalla akimjulia hali Mzee Francis Maige Ngosha aliyelazwa kwenye wodi ya Wanaume Hospitali ya Rufaa Amana leo jijini Dar es Salaam.


Mzee Francis Maige Ngosha (kwenye kitanda) akitolewa katika Hospitali ya
Rufaa Amana tayari kwa kupelekwa Hosptali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.



Naibu Waziri Dk. Hamisi Kigwagalla akiongea na waandishi wa habari kuhusu hatua waliyochukua ya kumuhamishia Mzee Maige kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga akizungumza na Mzee Francis Maige mara baada ya kupakiwa kwenye gari ya kubeba wagonjwa tayari kwa kupelekwa Muhimbili leo jijini Dar es Salaam.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget