Na Tiganya Vincent, Tabora
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri awaagiza wafanyabiashara wote
walioko katika eneo la machimbo ya dhahabu Kitunda wilayani Sikonge
kuhakikisha wanakuwa na maeneo ya kuhifadhi taka ngumu na laini kwa
ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali hasa yale ya mlipuko.
Mkuu
wa Mkoa huyo alitoa agizo hilo jana wilayani humo wakati anaongea na
wakazi wa Kitunda wanajihusisha na uchimbaji wa dhahabu au utoaji wa
huduma za vinjwaji na chakula machimboni hapo.
Alisema
kuwa hakuna hatakayeruhusiwa kuendesha shughuli zake mbalimbali ziwe za
uchimbaji au biashara chakula na vinjwaji kama hatakuwa amechimba choo
na kuweka kifaa cha kutupa mabaki ya taka ngumu na laini.
Bw.
Mwanri aliongeza kuwa eneo hilo linahitaji usafi wa hali ya juu kwa
sababu ya idadi kubwa ya watu wanaoishi katika eneo hilo ambapo inaweza
kusababisha maafa itatokea mtu mmoja akaugua ugonjwa wa mlipuko kama
vile kipindupindu aliweza kuwaathiri watu wengi na wakati mwingine
kusababisha maafa ambayo yanaweza kuzuilika.
“Hapa
lazima tuhakikishe usafiri wa hali ya juu kwani tusipofanya hivyo
tunaweza kufa kama kuku waliougua ugonjwa wa kideli …uongozi huu hako
tayari kuona mtu anafanyabiashara katika mazingira hatarishi kwa wateja
wake”alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Aidha
, Mkuu huyo wa Mkoa aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Sikonge kuleta Pipa kubwa la kutupa taka ili kulinda mazingira ya eneo
hilo.
Kwa
upande wa wachimbaji wa eneo hilo amewaagiza kujiwekea taratibu za
kutozana faini kwa watu wanachafua mazingira kwa ajili ya kuhakikisha
afya zinaendelea kuwa salama na magonjwa ya mlipuko na hivyo kuendelea
na shughui za uchimbaji madini pindi watakaporuhusiwa.
Post a Comment