Waziri wa Kilimo, Maliasili,
Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed (kushoto)
akimkabaribisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya
Kilimo ya Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kulia) wakati
walipomtembelea Ofisini kwake mjini Unguja.
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara
wa TADB, Bw. Augustino Chacha (wapili kushoto) akikaribishwa na Waziri
wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid
Mohamed (kulia) wakati viongozi wa TADB walipomtembelea Mhe. Waziri
Ofisini kwake mjini Unguja. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa TADB, Bw. Francis Assenga (wapili kulia) na Meneja Mikopo wa TADB,
Bw. Samuel Mshoto.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi Maryam Juma Abdullah
(aliyesimama) akizungumza wakati ugeni kutoka TADB ulipomtembelea Waziri
wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid
Mohamed Ofisini kwake mjini Unguja.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akieleza dhima ya Benki ya Kilimo
wakati walipomtembelea Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed (wapili kulia).
Waziri wa Kilimo, Maliasili,
Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed (aliyesimama)
akizungumza na ugeni kutoka TADB. Katika mkutano huo Mhe. Waziri
aligusia fursa lukuki za uwekezaji katika kilimo visiwani Zanzibar.
Waziri wa Kilimo, Maliasili,
Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed (aliyesimama
katikati) akifafanua kuhusu sursa za za uwekezaji zilizopo Zanzibar
wakati wa mkutano wake na ugeni kutoka TADB. Wengine pichani ni Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (kushoto) na
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili
Bibi Maryam Juma Abdullah (kulia).
Waziri wa Kilimo, Maliasili,
Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed (aliyesimama)
akihimiza kuhusu umuhimu wa TADB kuwekeza Visiwani humo. Kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi
Maryam Juma Abdullah.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akitoa ufafanuzi kuhusu masuala
mbalimbali juu ya huduma za Benki ya Kilimo kwa Waziri wa Kilimo,
Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed (kulia).
Kushoto Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha.
Ugeni wa Benki ya Kilimo wakiwa
katika ya pamoja na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
Zanzibar na maafisa wa Wizara hiyo.
…………………………………
Na Mwandishi wetu,
Waziri wa Kilimo, Maliasili,
Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed amesema sasa ni
wakati muafaka kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB)
kuwekeza Visiwani Zanzibar ili kuchagiza juhudi za Serikali za
kuwawezesha kiuchumi wakazi wa visiwa hivyo wanaojishughulisha na sekta
za kilimo, uvuvi na uchakataji mazao.
Mhe. Hamad amesema Visiwa vya
Zanzibar vina maeneo mengi ya uwekezaji yenye kuweza kuongeza tija na
ongezeko la uchumi visiwani humo ikiwa kutakuwa na uwekezaji mkubwa
katika maeneo hayo.
“Nawahakikishia, mkianza kuwekeza
katika miradi kama ya mwani, uvuvi na karafuu Bebki itapata matokeo
makubwa sana na mnaweza kuitumia Zanzibar kama mfano rejea katika utoaji
wa mikopo yenye tija nchini,” alisihi.
Kwa mujibu wa Mhe. Waziri,
Zanzibar ni miongoni mwa visiwa vyenye utajiri mkubwa ambavyo kukiwa na
uwekezaji wa kimkakati vinaweza kutokea matokeo makubwa na yenye
kuwanufaisha wananchi wengi.
Akizungumza na Mhe. Waziri, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema Serikali
iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili
kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha
upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi
katika kilimo nchini.
Bw. Assenga ameongeza kuwa Benki
inatambua fursa za uwekezaji Visiwani Zanzibar na amemuahidi kuwa
wamejipanga kuanza uwekezaji mkubwa wa wadau wa sekta za kilimo na uvuvi
ambazo ni sekta za kipaumbele zinazopatiwa mikopo na TADB.
Ameongeza kuwa Benki yake
imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa sekta hizo ili kuongeza
tija sekta hizo ili kupambana na umaskini nchini.
TADB ni taasisi ya serikali ambayo
ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha
mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa unachangiwa
kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa
zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya
kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia
hali halisi ya sekta ya kilimo na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi
kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Post a Comment