Wakala wa Vipimo Mkoa wa
Lindi imezuia matumizi ya mizani 94ya vyama vya msingi vya
ushirika(AMCOS) katika Wilaya ya Ruangwa. Mizani hiyoimezuiwaisitumike
katika msimu ujao wa ununuzi wa ufuta/korosho mpaka itakapofanyiwa
marekebisho na Mafundi Mizani kwa kurekebisha mapungufu yaliyoainishwa
na Wakaguzi wa mizani hiyo,ambapo Mizani hiyo itakaguliwatena na Maafisa
vipimo mara baada ya matengenezokukamilika na endapo Mizani hiyo
itakidhivigezoitagongwamuhuri na kubandikwa stika maalum
ndipozitaruhusiwa kutumika wakati wa msimu.
Katika zoezi la ukaguzi wa Mizani
kwenye Wilaya ya Ruangwa Wakala wa Vipimo imehakiki jumla ya vyama vya
ushirika vya msingi (AMCOS) 23 na kukagua jumla ya mizani 150 ambapo
kati ya mizani hiyo iliyopimwa na kuhakikiwa kuwa sahihi ni mizani 56 na
iliyozuiliwa kutumika mpaka itakapofanyiwa marekebisho ni mizani 94.
Mizani mingi imeonekana kuwa na
mapungufu (haipimi sahihi) kwakuwa ilibainika baadhi ya mizani ina
mapungufu kuanzia 200g hadi 1kg ambayo kwa kawaida mzani unatakiwa kuwa
na Upungufu unaokubalika wa kiasi cha 80g tu. Vilevile baadhi ya mizani
imechakaa na kupelekeakupoteza usahihi katika Upimaji wake kutokana na
namna mizani hiyo inavyohifadhiwa kwani huifadhiwa katika maeneo machafu
yenye vumbiambayo husababisha mizani kupata kutu, pia njia
inayotumikakusafirishia mizani hiyo sisalama kwani mizani husafirishwa
kwa Usafiri wa pikipiki ambao husababisha mzani kuangusha baadhi ya
vifaa vyakemuhimu.
Meneja wa Mkoa Wakala wa Vipimo
Lindi Bw. Stephen Masaweameeleza kuwa “tumeamua kuendeshea zoezi hili la
ukaguzi wa mizani ili kubaini mizani iliyo sahihi na kuipitisha na
kwaile itakayohitaji marekebisho mafundi
watapitakuifanyiaukarabatikishatutaihakiki upya na kama itakuwa sawa
tutaipitisha.
Zoezi hili litapunguzasana gharama za uendeshaji wa vyama
vya ushirika vya msingi kwani awali mafundi mizani walikuwa wanapita na
kurekebisha mizani zote, hii ilikuwa inapelekea nyama vya ushirika vya
msingi kutumia gharama kubwa ya matengenezo hadi Tsh. 400,000= kwa mzani
Mmoja lakini kwa sasa mafundi watapita kurekebisha mizani iliyobainika
kuwa na mapungufu ambayo yameainishwa na Wakaguzi wa mizani tu.”
Masawealisema, zoezi hili la
ukaguzi wa mizani (kapani) ya vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS)
lilianzia katika Wilaya ya Ruangwa nasasa zoezi hilo linafanyika katika
Wilaya ya Nachingwea.zoezihili la ukaguzi wa Mizani ni endelevu na
litafanyika pia katika Wilaya zilizobakia ambazo ni Wilaya zaLiwale,
Kilwa, Lindi Mjini na Lindi Vijijini kwa kuhakiki mizani zote za vyama
vya ushirika vya msingi.
Pia, baadhi ya wananchi
wameipongeza sana Wakala wa Vipimo kwa kuwapa elimu ya matumizi sahihi
ya Vipimo pamoja na kufanya ukaguzi wa Mizani kabla ya mafundi kupewa
tenda ya kuitengeneza na Halmashauri, Miongoni mwao ni ndugu Laurent
Adrian Muyaambae ni mwanakijiji wa Michenga A na ni karanimpimaji kwenye
ghala la Michenga A.
Wakala wa Vipimo inatoawito kwa
wakulima wote wa ufuta na Korosho kuhakikisha kuwa wanauza mazao yao
katika vituo vyenye mizani iliyohakikiwa na Wakala wa Vipimo na
kupigwachapa ya bibi na bwana na kuweka tarakimu mbili za mwaka husika
(17) kwa mwaka huu, na tumeanza kuweka stika maalum ya Wakala wa Vipimo
mbele ya mizani yote iliyohakikiwa na Wakala wa Vipimo. Pia wahakikishe
kuwa wanasoma kilo za mazao yaopindiwanapoenda kupima katika maghala na
si kwa kumuaminikarani tu akishakusomea kwani wengine husoma kilo
pungufu kwa ajili ya kuwapunja mazao yao.
Post a Comment