Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto
wa miaka 12, Dorcas Meshak mkazi wa kitongoji cha Mbughantigha kijiji
cha Matongo tarafa ya Ikungi, ameuawa na watu wasiojulikana na
kunyofolewa baadhi ya viungo vyake.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kaimu
Kamanda Jeshi la Polisi mkoani hapa, SSP Isay Mbugh alisema Mei, 18
mwaka huu saa sita mchana wakati ambao Dorcas alipoondoka nyumbani kwao
kwa lengo la kwenda shambani kuchuma mahindi, umbali wa kilometa 70.
Alisema mtoto huyo amenyofolewa macho yote mawili, kukatwa matiti yote na kuondolewa sehemu zake za siri.
“Mtoto Dorcas hakuweza
kurudi nyumbani kitendo kilichosababisha ipigwe yowe ili watu
wakusanyike kwa ajili ya kumtafuta. Haikuchukua muda mrefu, mwili wa
Dorcas ulikutwa ukiwa umenyongwa hadi kufa kwa kamba ya ngozi,” alisema.
Alisema uchunguzi wa awali umebaini
kuwa mauaji hayo yanahusishwa na imani za ushirikina na hadi sasa hakuna
watu waliokamatwa kuhusiana na mauaji hayo.
Katika tukio la pili, Kaimu Kamanda
Mbugh, alisema watu wawili wamepoteza maisha kufuatia kutokea ajali ya
gari anina ya Noah, tukio ambalo lilitokea Mei, 20 mwaka huu saa 6.45
mchana huko katika kijiji cha Mwaja tarafa ya Unyankumi Manispaa ya
Singida.
“Ajali hiyo imehusisha noah T.402
DFH iliyokuwa ikiendeshwa na Said Shaban (33), na chanzo cha ajali ni
mwendo kasi kitendo kilichosababisha ashindwe kulimudu. Waliofariki
kwenye ajali hiyo,ni Elia Daniel (34) mkulima kijiji cha Mwankoko na
mwanamke mmoja ambaye jina wala makazi yake,hayajafahamika,” alisema.
Aidha, aliwataja majeruhi wa ajali hiyo
kuwa ni Mratibu Elimu kata ya Mtamaa, Nicodem Elias (45), Juma
Ramadhan, mwalimu Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, Elia Bilau mkulima na
mkazi wa Magungumka Kapela Donad (28).
Kaimu kamanda huyo, alisema dereva wa
Noah hiyo Said Shaban anashikiliwa na Jeshi la Polisi na upepelezi
ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Post a Comment