Kivuko kipya cha MV KAZI kikiwasili kwa mara ya kwanza upande wa Magogoni tayari kwa majaribio ya kubeba abiria na magari.
Magari yakiingia kwa mara ya
kwanza kwenye kivuko kipya cha MV KAZI tayari kuvuka kuelekea upande wa
Kigamboni. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio baada ya ujenzi
wake kukamilika.
Abiria wakiingia katika kivuko
cha MV KAZI tayari kwa kuvuka kuelekea upande wa Kigamboni. Kivuko hicho
kilikua kikifanyiwa majaribio ya kubeba abiria kwa mara ya kwanza baada
ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
Abiria wakiingia katika kivuko
cha MV KAZI tayari kwa kuvuka kuelekea upande wa Kigamboni. Kivuko hicho
kilikua kikifanyiwa majaribio ya kubeba abiria kwa mara ya kwanza baada
ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
Kivuko cha MV KAZI kikiondoka kwa
mara ya kwanza kutokea Magogoni kuelekea Kigamboni kikiwa na abiria na
magari. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio mara baada ya ujenzi
wake kukamilika kabla ya kukabidhiwa kwa TEMESA.
Kivuko cha MV KAZI kikielea kwa
mara ya kwanza majini huku kikiwa na abiria na magari, kivuko hicho
kilikua kikifanyiwa majaribio baada ya ujenzi wake kukamilika hivi
karibuni.
Abiria wakishuka kutoka katika
kivuko cha MV KAZI mara baada ya kuwasili upande wa Kigamboni kwa
majaribio, ujenzi wa kivuko hicho umekamilika na kinategemewa kuanza
kutoa huduma hivi karibuni.
……………………….
ALFRED MGWENO
Kivuko cha MV KAZI hatimaye
kimefanyiwa majaribio ya kubeba abiria na magari kwa mara ya kwanza
baada ya kukamilika kwa matengenezo yake. Majaribio hayo yalifanyika
kulingana na sheria na taratibu za vyombo vya majini ambayo inavitaka
vyombo vyote vya majini kufanyiwa majaribio kabla ya kuanza kazi ili
viweze kupatiwa cheti cha ubora “Seaworthiness Certificate”.
Awali wataalam kutoka Chuo cha
Ubaharia Dar es Salaam (DMI) waliweza kupima ubora na uimara wa kivuko
hicho kwa kutumia utaratibu wa kuweka mawe yenye kilo zinazolingana na
uwezo wa kivuko pamoja na magunia ya mchanga ili kuweza kupima uwezo wa
kivuko kulingana na mahitaji yaliyoainishwa kabla hakijabeba abiria na
mizigo. Zoezi hili pia lilihusu kufanyika kwa kipimo cha kuhakikisha
kuwa kivuko hakilali upande mmoja yaani “Inclination test” ambapo
kilionyesha Kivuko kiko sawa.
Taarifa ya zoezi hili itakuwa sehemu ya
vitu vya makabidhiano wakati wa upokeaji wa Kivuko.
Miongoni mwa waliokuwepo
kushuhudia majaribio hayo alikuwa Mkuu wa Vivuko Magogoni/Kigamboni,
Mhandisi Lukombe King’ombe ambaye alisifu uwezo wa kivuko hicho na
kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha wanakitunza kivuko hicho
kwani kitawasaidia kupunguza msongamano wa abiria na magari hasa majira
ya asubuhi na jioni.
Ujenzi wa MV KAZI umegharimu
Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo wa kubeba abiria 800
magari 22 sawa na jumla ya tani 170. Kivuko hicho kitakabidhiwa rasmi
hivi karibuni kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa ajili ya kuanza
kutoa huduma. Aidha ujio wa kivuko hicho utaongeza idadi ya vivuko
kufikia vitatu vitakavyotoa huduma ya kuvusha abiria na magari katika
eneo la Magogoni/Kigamboni.
Post a Comment