Na Husna Saidi & Nuru Juma
Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi
na Jeshi la KujengaTaifa inampango wakuunda kikosi kazi cha kupitia
changamoto zinazowakabili Wanafunzi wanaomaliza kidato cha Sita
kutojiunga na mafunzo yaJeshi kama sheria ya Jeshi la kujengaTaifa
inavyotaka.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini
Dodoma na Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Hussein Mwinyi alipokuwa akijibu
swali la nyongeza lililoulizwa na George Huruma Mkuchika Mbunge wa jimbo
la Newala Mjini.
Dkt. Mwinyi alisema kuwa Sheria ya
Jeshi la Kujenga Taifa ya mwaka 1964 imeweka ulazima wa vijana wa
Tanzania wanaomaliza kidato cha sita kujiunga na mafunzo ya Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa Sheria, hatahivyo mwaka 1994 Serikali
iliyasitisha kwa muda mafunzo hayo na kuyarejesha tena mwaka 2013 na
yanaendelea hadi sasa.
“Takwimu zilizopo zinaonyesha
kupungua kwa idadi ya vijana wanaojiunga na mafunzo hayo muhimu ya jeshi
la kujenga Taifa hali hii imesababishwa na changamoto mbalimbali ikiwa
ni pamoja na kugongana kwa tarehe za kuanza mafunzo ya vijana kwa mujibu
wa sheria na kufunguliwa kwa vyuo mbalimbali hapa nchini ambapo mihula
ya mafunzo huanza”, alisema Dkt. Mwinyi.
Aidha alisema hali hiyo imewafanya
vijana wengi walioteuliwa kujiunga na vyuo kukosa nafasi ya kujiunga na
mafunzo ya JKT kwamujibu wa sheria na changamoto nyingine ni ubovu wa
miundombinu, rasilimali watu na pamoja na fedha, hatahivyo Serikali
inaendelea na juhudi za kupata suluhu ya changamoto hizo.
Dkt. Mwinyi aliongeza kuwa mwaka
2014 vijana waliohitimu kidato cha sita walikuwa 41,968 na kati yao
waliojiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa walikuwa 31,692 ambao
ni sawa na asilimia 75.5.
Aidha mwaka 2015 kulikuwa na
wahitimu 40,753 na waliojiunga ni 19,990 sawa na asilimia 48.8 huku
mwaka 2016 wahitimu kidato cha sita walikuwa 63,623 waliojiunga na Jeshi
ni 14,747 sawa na asilimia 23.2.
Zoezi la kuwachagua vijana hao
kujiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa halina vigezo maalum kwani
kila kijana aliyemaliza kidato cha sita anasifa ya kujiunga na mafunzo
hayo.
Post a Comment