Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

WANAFUNZI WATATU WAFA MAJINI MKOANI GEITA


Baadhi ya viongozi wa kiserikali na wakidini pamoja na wananchi wakiwa kwenye ibada ya mazishi ya  watoto watatu ambao wamekufa maji .

Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita waki shuhudia miili ya marehemu .

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akitoa pole kwa wafiwa wa tukio la watoto watatu ambao wamekufa kwenye maji ziwa Viktoria.

Mkuu wa Mkoa wa  Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga  akitoa pole kwa wafiwa wa tukio la watoto watatu ambao wamekufa kwenye maji ziwa Viktoria.

Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye eneo la tukio.

Usafiri wa Boti ambao wamekuwa wakitunmia wanakijiji wa Kisiwa cha Lulegea ambacho ndio kiliwaacha wanafunzi kabla ya tukio kutokea.

 Baadhi ya abilia wakishuka kwenye kivuko hicho.

Mkuu wa Mkoa wa  Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga  akizungumza na wananchi wa Kisiwa cha Lulegea.

Baadhi ya watoto ambao wamenusurika wakati wa dhoruba ambalo lilitokea





Kufuatia
tukio la wanafunzi 24 kuzama maji  ziwa
viktoria na wengine watatu kupoteza maisha wakati wakitokea masomoni  Kijiji cha Butwa na wakielekea    Kitongoji cha Lulegea  Kata ya
Izumacheli Wilaya na Mkoa wa Geita,Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu
Ezekiel Kyunga ameagiza halmashauri ya Wilaya pamoja na wananchi wa kijiji
hicho kuwa na  ushirikiano ili kujenga
shule kwenye kisiwa hicho.
Hayo
ameyasema wakati alipokuwa akitoa pole kwa wafiwa na jamii ambayo ipo kwenye
kisiwa hicho kutokana na tukio la kufariki kwa wanafunzi watatu wa shule ya
msingi Butwa wakati wakitokea shule kurudi Nyumbani.
 
Mh,Kyunga
amesema kuwa ili kuwasaidia wananchi wa Kitongoji cha Lulegea hawana budi
kujenga shule na kwamba wakati utakapokuwa umetulia wa mvua ni vyema kwa
wananchi kujumuika kwa pamoja na kushirikiana ili waweze kujenga shule ambayo
itawasaidia wananfunzi.
 
“Mimi  pia nimesikitishwa sana na msiba huu wa
wanafunzi hawa lakini ni muhimu kutafuta suluhisho la matatizo haya kwa  wanafunzi  na suluhisho ni serikali na nyie wananchi
kujitokeza kuchangia nguvu ili tuweze kujenga shule kwenye eneo hili ili
matatizo ya namna hii yasiweze kujirudia tena siku nyingine”Alisema Kyunga.
 
Tululaza
Kurulahenda ambaye alikuwa amewabeba wanafunzi hao kwenye Mtumbwi ambao ulizama
ameelezea kuwa chanzo ambacho kilisababisha ajali hiyo ni kutokana na  watoto kutokutulia wakati akiendesha
mtumbwi  pamoja na hali kutokuwa shwari
ya ziwani.
 
“Muda
ulikwenda sana na boti ambayo huwa inawabeba wanafunzi ilikuwa
imekwisharudi  moja kati ya mama ambaye mtoto
wake amefariki akaniomba niwafuate na mtumbwi namimi sikubisha kwakuwa walikuwa
ni watoto ikabidi niwafuate kwa bahati mbaya wakati ninarudi nikiwa nimekaribia
kufika upande wa pili hali iliharibika na kukawepo na upepo hali ambayo
ilipelekea wanafunzi kuanza kupiga kelele na kuruka lakini hata hivyo mimi
pamoja na mwanafunzi ambaye anaitwa Tisekwa tulianza juhudi za kuwaokoa wengine
ndipo  na tukawa tumefanikisha baada ya
baadhi ya wavuvi wenzangu kuja kutusaidia na tulipowaokoa tukagundua kuwa
watatu hawaonekani ndipo tukaanza mchakato wa kuwatafuta baada ya juhudi majira
ya saa moja tukaupata mwili wa mwanafunzi mmoja akiwa amefariki wengine
tumewapata asubuhi”Alisema huku akiwa na masikitiko Tululaza.
 
Aidha
Tisekwa Gamungu ambaye ni mtoto aliyewaokoa wenzake amesema kuwa walikuwa
wakitoka shuleni  wakati wakiwa njiani  wakirudi waliona kama kimbunga kimetokea hali
ambayo ilipelekea wengi wao kulia huku wakiombwa kurudishwa kule ambako
wametokea.

Wanafunzi
ambao wamepoteza maisha kwenye tukio
hilo ni Kumbuka Bruno Thomas (13) ni
mwanafunzi wa darasa la tano  ,Anastazia Christopha (12)darasa la tatu na
Sophia Muungano (11)darasa la pili
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget