Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo inapenda kutolea ufafanuzi hoja ya Mbunge wa Ubungo Mhe.
Saed Kubenea kuhusu kukabidhiwa Uwanja wa Taifa ukiwa haujakamilika.
Ukweli ni kwamba Uwanja wa
Taifa umejengwa kulingana na usanifu (design) wake kwa kufuata vigezo
vya FIFA na Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF) na kukamilika
ambapo vyombo vyote vya serikali vilikagua na kujiridhisha kulingana na
makubaliano ya mkandarasi.
Uwanja wa Taifa umejengwa kwa
mtindo wa kipepeo hivyo wakati wa mvua hususani yenye upepo mkali
hupelekea maji kufika katika maeneo ya majukwaa likiwemo jukwaa kuu
(VVIP) na sio kuwa uwanja huo unavuja.
Ujenzi wa Uwanja huo uligharimu kiasi cha shilingi Bilioni 56 mpaka kukamilika kwake.
Hata hivyo Wizara kwa
kushirikiana na mshauri mwelekezi wamekubaliana kuweka paa eneo la
jukwaa kuu (VVIP) ili kuepusha maji kuingia katika eneo hilo kipindi cha
mvua.
Imetolewa na:
Genofeva Matemu
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
09/05/2017
Post a Comment