Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo leo Mei 25, 2017
amekutana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias
Andengenye na kufanya nae mazungumzo ofisini kwake.
Katika mazungumzo yao wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kufanya kazi na pia jeshi la zimamoto na uokoaji wameomba ushirikiano toka kwa mkuu wa mkoa ili kuweza kuliunganisha jeshi hilo na mamlaka za serikali za mitaa ili liweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi kwani mnufaika mkubwa wa huduma zao ni mamlaka hizo husika.
Gambo ametoa rai kwa Jeshi hilo kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala ya kusubiri matukio ya ajali za moto kutokea wanapaswa kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuyazuia matukio hayo na kwa kufanya hivyo watapunguza sana kazi yao kwani majanga ya moto yatakua historia.
Pia wamekubaliana kuhakikisha ramani za majengo na michoro ya mpango kabambe (master plan) kwa jiji la Arusha zinapitiwa, lengo ni kuona mapungufu ya kiusalama dhidi ya majanga ya moto na kuona namna ya kuzitatua mapema.
Mkoa wa Arusha hasa kwa jiji la Arusha ni miongoni mwa maeneo ambayo kuna changamoto kubwa sana hasa panapotokea majanga ya moto kwani miundo mbinu na vituo vya zimamoto havitoshelezi mahitaji.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia) akiwa katika mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (wa pili kulia) alipokutana nae ofisini kwake leo. Wengine ni Kamisha Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Arusha, Ali Dady (kushoto) pamoja na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha, Bakari Mrisho
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye walipokuwa katika mazungumzo ofisini kwake leo.
Baadhi wa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakifatilia mazungumzo hayo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (kushoto), Kamisha Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Arusha, Ali Dady (wa pili kulia) pamoja na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha, Bakari Mrisho baada ya mazungumzo. Picha zote na James Mhilu, Arusha.

Post a Comment