Naibu
Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Tekeme , ambaye pia ni Diwani wa
kata ya Temeke, Feysali Salum , akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kumalizika kwa fainali hizo za michuano ya Drafti
Mkoa wa Dar es salaam zilizofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Jijini Dar
es salaam. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Mstahiki Meya wa jiji la Dar
es Salaam Isaya Mwita.
Naibu meya wa Halmshauri ya Manispaa ya Temeke, mbaye pia ni Diwani wa kata ya Temeke, Feysali, (mwenye shati damu ya mzee)
akifuatilia kwa makini fainali za michuano ya mchezo wa Drafti Mkoa wa
Dar es salaam, zilizofanyika jana viwanja vya Mwembe Yanga Wilayani
Temeke Jijini Dar es salaam .
Naibu
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala , ambaye pia ni Diwani wa kata
ya Temeke, Feisali Salum, akizungumza na waandishi wa
habari mara kwaniabaya ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya
Mwita baada ya akumalizika kwa fainali hizo za michuano ya Drafti
Mkoa wa Dar es salaam zilizofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Jijini Dar
es salaam.
Naibu Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, amabaye pia nia Diwani wa kata ya
Temeke
Feysali Salum, akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi
zawadi kwa washindi wa michuano hiyo,katika mashindano hayo mshindi wa
kwanza aliata zawadi ya pesa tathilim sh.200000/, , wapili 100, 000 na
watatu 50,000.
Mratibu wa mashindano ya fainali ya michuano ya mchezo wa Drafti
Mkoa wa Dar es salaam, (Draft Compitition) Jamali Deogratus, akizungumza
na waandishi wa habari kalba ya fainali hizo kufanyika huku akitoa
maelekezo pamoja na faida za mchezo huo kwa jamii na wadau mablimbali wa
mchezo wa Drafti hapa nchini.
NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MASHINDANO ya mchezo wa Darfti ya Mstahkimi Meya wa
jiji la Dar es Salaa Isaya Mwita yamemalizika jana na kufungwa na Naibu Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Feysali Salum ambapo jumla ya washindi wa tatu waliibuka
kidedea na kunyinyakulia zawadi kila mmoja.
Mashindano hayo ambayo yalianza Mei 13 na
kufunguliwa na Meya Mwita yalikuwa na jumla ya washiriki 64, yalifkia tamati
hiyo jana ambapo mshindi wa kwanza Kiraba Ngibombi ambaye pia ni Mweyekiti wa
cahama cha mchezo wa Drafti mkoa wa Dar es Salaam alipata pesa tathilisimu
sh.200, 000.
Aidha mshindi wa pili katika mashindano hayo ni
Willium Mgata , maarufu kama Bad Face ambaye alijinyakulia kitita cha sh.100,000
na mshindi wa tatu alikuwa ni Hossein Ally aliyapata zawadi ya sh.50,000.
Akikabizi zawadi hizo kwa niaba ya Mstahiki Meya wa
Jiji, Naibu Meya wa Temeke ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Temeke kupitia Chama
Cha Mapinduzi CCM , Feysali pamoja na
mambo mengine alimpongeza Meya Mwita kwakuanzisha mashindano hayo na kuahidi
kumuunga mkono.
Naibu Feysali alisema kwamba kutokana na umuhimu
aliouonyesha mstahiki Meya wa jiji, atashirikiana nae ili kuwa wawalezi wa
chama hicho na hivyo kuwawezesha kwenye mchezo huo.
“ Nampongeza Mstahiki Meya wa jiji kwa kuliona hili
jambo, pia kutoa heshma kubwa kulifanya ndani ya kata yangu, amefanya jambo
zuri sana, sasa kwa umuhimu huo nipo tayari kumuunga mkono, nitashirikiana nae
ili kuwa walezi wa chama hichi” alisema Naibu Feysali.
Aliongeza kuwa,”
nataka ifikie mahala, muwe mnaenda kushindana hata mikoani, jambo ambalo
kwakushirkina na Mstahiki Meya wa jiji Mwita, Mbunge wa jimbo hili Abdala
Mtolea, tutawadhamini , muda wowote ambao mtahitaji nyie” alisisitiza.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa chama cha mchezo huo
ambaye ndie aliibuka mshindi wa kwanza Kiraba, alisema kuwa alichokifanya
Mstahiki Meya wa jiji ni kufungua njia ya mchezo huo na hivyo kusisitiza kwamba
kufanyika kwa usajili wa chama hicho.
“ Tunampongeza sana Meya wa jiji kwa kuweza
kufanikisha jambo hili, limeonyesha msisimko mkubwa, watu wengi wamejitokeza,
hii ni heshma kwake, kwenye mengine kutakuwa
na hamasa kubwa zaidi kutokana na hili lililofanyika leo” alisema Kiraba.
Mashindano ya mchezo wa Drafti yalidhaminiwa na
Mstahiki Meya wa jiji Mwita , ikiwa na lengo la kuhamasisha michezo mingine
iweze kufahamika kama ilivyo kwenye mpira wa miguu na michezo mingine.
Post a Comment